Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa Elimu ya Pensheni kwa wâfânyakazi wa TÂZARA.
Lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha wânâchama kuhusu kanuni mpya ya kukokotoa pensheni ya Uzeeni.
Akizungumza na wafanyakazi hao Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa NSSF, Christina Kamuzora alisema kuwa kanuni hiyo imekwishaanza kutumika na kuwahakikishia kwamba malipo yao ya pensheni yatatolewa kwa uharaka zaidi kwa kuwa huduma zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Kamuzora akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA (hawapo pichani), wakati wa utoaji wa elimu kwa wafanyakazi hao.
Wafanyakazi wa TAZARA wakimsikiliza Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Kamuzora (hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment