Mkuu wa mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi leo amemkabidhi Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Msenza Mwenge wa Uhuru utakaokimbizwa kwa siku 5 mkoa wa Iringa kwenye halmashauri 5 na kuzindua miradi, kukagua na kuweka jiwe la Msingi. leo Mwenge huo umekimbizwa Wilaya ya Mufindi , kesho wilaya ya Iringa. shamrashamra hizo zilifanyika kijiji cha Nyigo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akipokea Mwenge wa Uhuru utakaokimbizwa kwa siku 5 mkoa wa Iringa kwenye halmashauri 5 na kuzindua miradi, kukagua na kuweka jiwe la Msingi katika maeneo yaliyowekwa, leo hii katika kijiji cha Nyigo.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiushika Mwenge huo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kilolo Selemani Mzee, wakati wa hafla ya kuupokea Mwenge kutoka Mkoa wa Njombe leo eneo la Nyigo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mkuu wa wilaya ya Kilolo Selemani Mzee na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jolwika Kasunga wakicheza ngoma ya kihehe wakati wa hafla ya kuupokea Mwenge kutoka Mkoa wa Njombe leo eneo la Nyigo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Selemani Mzee akiushika Mwenge huo.
Vijana wa Karate na chipukizi kutoka Iringa wakiwaonyesha Njombe ufundi wa kisansui.
No comments:
Post a Comment