Thursday, June 16, 2016

MRADI WA AACES WAONYESHA THAMANI YA ASASI ZA KIRAIA NCHINI TANZANIA.

Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay akizungumza jijini Dar es Salaam Juni 15, 2016 katika uzinduzi wa ripoti ya mashirika ya mashirika yasiyo ya kiserikali katika kufunga miradi uliyokuwa unafadhiliwa na watu wa Australia kupitia mpango unaojulikana kwa jina la Australia - Africa Community Engagement Scheme (AACES) Tanzania, utakaofikia mwishoni Juni 30, 2016. AACES ulikuwa ni mradi wa miaka mitano, wa ushirikiano baina ya serikali ya Australia na Mashirika kumi yasiyo ya kiserika nchini humo pamoja na washirika wao walioko barani Afrika. Mradi huu umekuwa ukitekelezwa katika nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
 Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa ripoti Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi hati ya umiliki wa bajaji vijana walioweza kusimamia vyema mradi wa AACES wa Marie Stopes Tanzania. Pembeni (aliyeshika kipaza sauti) ni Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay na Meneja wa mrasi huo wa Marie Stopes Bi. Lilian Charles. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam Juni 15, 2016 katika uzinduzi wa ripoti ya mashirika ya mashirika yasiyo ya kiserikali katika kufunga mradi uliyokuwa unafadhiliwa na watu wa Australia kupitia mpango unaojulikana kwa jina la Australia - Africa Community Engagement Scheme (AACES) Tanzania, utakaofikia mwishoni Juni 30, 2016.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa ripoti Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akiongea machache kabla ya kuzindua ripoti ya mashirika ya mashirika yasiyo ya kiserikali katika kufunga mradi uliyokuwa unafadhiliwa na watu wa Australia kupitia mpango unaojulikana kwa jina la Australia - Africa Community Engagement Scheme (AACES) Tanzania, utakaofikia mwishoni Juni 30, 2016.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa ripoti Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akikata utepe ili kuashiria uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa ripoti Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya (katikati) akioyesha ripoti mara aada ya kumaliza kuzindua.
Mratibu wa Mradi wa AACES - Caritas Tanzania, Joseph Masago akiwatambulisha baadhi ya wananchi wa Lindi walioweza kufaidika na mradi huo.
Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay (kushoto) na Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa ripoti Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya w akifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Meneja wa Usimamizi wa Mradi wa Mama na Mtoto wa Kilindi, Bw. Daudi Gambo akizungumza machache kuelezea jinsi mradi  huo ulivyokuwa msaada kwa wakazi wa Kilindi na maeneo ya jirani.
Wasimamizi wa mashirika wakitoa shuhuda zao.
Wasimamizi wa mashirika wakitoa shuhuda zao. --- Zaidi ya wanawake milioni 2.3 pamoja na wanyonge katika mataifa 11 duniani kote, wamenufaika na miradi ya usalama wa chakula, huduma ya Afya ya mama na mtoto, maji na usafi wa mazingira kwa jamii na mashuleni, kwa ufadhili wa watu wa Australia kupitia mpango unaojulikana kwa jina la Australia - Africa Community Engagement Scheme (AACES) Tanzania, unaotakaofikia mwishoni Juni 30, 2016. AACES ulikuwa ni mradi wa miaka mitano, wa ushirikiano baina ya serikali ya Australia na Mashirika kumi yasiyo ya kiserika nchini humo pamoja na washirika wao walioko barani Afrika. Mradi huu umekuwa ukitekelezwa katika nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe. Nchini Tanzania, Programu hii inayofadhiliwa na watu wa Australia inatekelezwa katika mikoa ya Arusha, Pwani, Dar es Salaam, Dodoma, Lindi, Morogoro, Mtwara, Singida, Tabora na Tanga. Mradi umejikita katika ushirikishwaji wa jamii yenyewe kwa msaada wa asasi za kijamii katika kuleta mabadiliko yanayohitajika viwango vya huduma za afya ya mama na mtoto, kilimo chenye tija, pamoja na maji na mazingira. “AACES inatambua umuhimu wa kushirikiana na asasi za kiraia katika hatua zote za miradi ya maendeleo kwani huleta matokeo mazuri katika maendeleo, na imedhihirika kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yanaweza kufanya kazi pamoja kuwaletea wanyonge huduma zinazohitajika. Serikali ya Australia inatambua umuhimu wa kazi zinazofanywa na Mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni washirika wetu, katika kusaidia kuleta maendeleo.” Anasema Marc Innes-Brown, Katibu wa Kwanza Msaidizi, kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika katika Idara ya Mambo ya nje na biashara Mashirika yanayofadhiliwa na Watu wa Australia, yanafanya kazi na sekta binafsi kutoa huduma za afya ya uzazi ambazo ni endelevu na kwa bei nafuu kupitia Mradi wa Bajaji za bei nafuu kama njia ya kuwafikia watu maskini wanaoishi pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam, kwa kuwapelekea elimu na huduma za uzazi wa mpango. Baadhi ya madereva vijana waliokopeshwa Bajaji kwa ajili ya kuwapeleka watoa huduma kwenye vituo vya afya vilivyo katika maeneo ya pembezoni na kuwarudisha, kisha kuendelea na biashara, ambapo madereva hao wameweza kurudisha mkopo huo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na kutoa nafasi kwa awamu nyingine ya mpango huo. Leo madereva hawa vijana watakabidhiwa kadi zao ili kuwa wamiliki halali wa Bajaji hizo. Zaidi ya wateja 26,000 wameweza kufikiwa na huduma za uzazi wa mpango jijini Dar es Salaam kupitia mradi wa Bajaji kati ya Januari 2014 na juni 2015 na kipato cha madereva wa Bajaji kikaongezeka kwa Asilimia 55 (55%). “Faida kubwa niliyoipata hasa ni maarifa niliyoyapata kuhusu uzazi wa mpango..Hivi sasa ninajua kuhusu njia zote za uzazi wa mpango na hata namna nzuri ya kuelimisha vijana kuhusu uzazi wa mpango. Binafsi, nimejiwekea malengo yangu na ninajiamini kwamba nitayafikia kwa sababu ya elimu niliyonayo kuhusu uzazi wa mpango” anasema Jonas mmoja wa madereva wa bajaji ambaye pia ni baba wa Watoto wawili. Kwa upande wa Maji na usafi wa mazingira, ujenzi wa vyoo vya kisasa pamoja na visima vya maji mashuleni, umechangia kuongezeka kwa mahudhurio ya Watoto shuleni pamoja na kujiamini miongoni mwa wanafunzi hususan wasichana. Vyoo hivyo vya kisasa vina eneo la kunawia mikono, chumba cha kubadilishia wakati wa hedhi, tanuru la kuchomea taka, sehemu ya haja ndogo pamoja na mazingira rafiki kwa wenye ulemavu.  Katika mikoa ya Lindi na Mtwara, mradi umewezesha ugawaji wa mbegu bora za mazao ya Muhogo, Alizeti na Kunde pamoja na mbolea kwa wakulima wadogo 6,386 wakiwemo wanawake, wanaume na wenye ulemavu. Wanawake waliwezeshwa kuboresha Maisha yao kwa kujipatia kipato cha ziada kupitia mikopo ya vyama vya akiba na mikopo vijijin ili kuboresha biashara zao. “Mtumizi ya mbegu bora pamoja na njia za kilimo cha kisasa yamesaidia kuongeza mavuno ninayopata shambani kutoka kilo 50 za ufuta kwa ekari moja hadi kufikia kilo 260 kwa ekari,” anasema Mwajuma Omari ambaye ni mkulima mdogo wa mkoani Mtwara. Mbali na kuwa mkulima, Mwajuma pia anajishughulisha na ujasiriamali shughuli ambazo humuongezea kipato. “Kutokana na kujihusisha na shughuli mbalimbali, ninaweza kumudu mahitaji ya familia yangu.” She says. Mradi wa AACES pia umekuwa ukifanya kazi na asasi za kiraia kuhusu mabadiliko ya kisera kwa kutoa nafasi kwa jamii kupaza sauti zao kupitia mabaraza ya kijamii. Jumla ya wakazi 1,700 wa wilaya tano za mkoa wa Tanga walipata nafasi za kushiriki katika mabaraza haya ambayo yalitoa kipaumbele katika masuala ya afya ya uzazi, afya ya mama na motto pamoja na elimu ya makuzi kwa vijana; kwa kuhusianisha na malengo mapya ya maendeleo endelevu. “Ninawashukuru mashirika ya Save the Children, World Vision Tanzania na Utepe mweupe (White Ribbon) ambao waliandaa jukwaa hili ambalo linatoa nafasi kwa watu wenye ulemavu kusimama mbele za watu na kueleza changamoto zinazotukabili katika kupata huduma za afya na elimu.” Anasema Khalid Mohamed Mngulu, mlemavu wa ngozi – Albino ambaye aliwakilisha Tanzania kwenye mdahalo wa kimataifa kuhusu afya WHA, Geneva. Nchini Tanzania, mradi wa AACES unatekelezwa na mashirika ya CARE Tanzania, Caritas Tanzania, Marie Stopes Tanzania - MST, WaterAid Tanzania na World Vision Tanzania. Ripoti ya mwisho ya mradi wa AACES ambayo inazinduliwa leo, inapatikana kwenye tovuti ya DFAT: www.dfat.gov.au

No comments: