Sunday, June 19, 2016

MKUU WA MKOA WA DODOMA AANZA KUSHUGHULIKIA MGOGORO BAINA YA WANANCHI WA KIJIJI CHA IKENGWA KONDOA NA PORI LA AKIBA LA MKUNGUNERO

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akiwaonesha Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa Naakala ya tangazo la Serikali lililotangaza pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano wa kujadili mgogoro baina ya wanachi hao na pori la akiba katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Shaban Kissu (aliyesimama) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa huo katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mzee Mathayo wa kijiji cha Ikengwa akiishukuru serikali ya Rais Magufuli kwa kuanza kushughulikia mgogoro baina ya wananchi wa kijiji hiko na pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma ambapo kamati iliyohusisha wananchi, Pori la akiba Mkungunero na Uongozi wa Wilaya Kondoa iliundwa kumaliza mgogoro huo.
Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Kondoa, pori la akiba Mkungunero na Viongozi wa kijiji cha Ikengwa kinachopakana na pori hilo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma katikati ya Wiki ili kujadili namna ya kutatua mgogoro baina ya wanachi wa kijiji hiko na pori la Mkungunero.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (katikati) akiagana na Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa baada ya kumaliza mkutano wa hadhara juu ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero katikati ya Wiki ambapo mkuu wa mkoa ameunda kamati ya kumaliza mgogoro huo inayohusisha wananchi, Pori la Mkungunero na Uongozi wa Wilaya Kondoa na wananchi wameshukuru makubaliano yaliyofikiwa ya kutafutiwa maeneo mengine ya makazi, kilimo na mifugo (Juni 15, 2016).
Wakina mama wa jamii ya kibarbaigi wa kijiji cha Ikengwa Kondoa wakimshukuru Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana baada ya kufurahishwa na makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa hadhara ya kutafutiwa maeneo mengine ya makazi, kilimo na mifugo kwa lengo la kumaliza mgogoro wa wananchi hao na pori la Mkungunero.

No comments: