Friday, June 24, 2016

Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu kufanyika Diamond Jubilee jijini Dar Juni 26


Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu, Sheikh Othman Ally Kaporo (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Mashindano hayo yatafanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Sheikh Mohammed Ally Hassan(kulia) na Sheikh AllySendo.
Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
MASHINDANO ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Quraan, yanatarajiwa kufanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo Juni 23, 2016, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo, Sheikh Othman Ally Kaporo, amesema, mashindano hayo ambayo ni sehemu ya kutekeleza ibadaya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifa mbalimbali Duniani.
“ Kwa wale watakaojaaliwa, wanaweza kufika kwenye msikiti wa Mtoro ulioko Kariakoo, na kujionea jinsi vijana wadodo wanavyosoma Quraan, kila siku usiku, na Jumapili ndio mashindano yenyewe haswaa.’Alisema.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, washindani watatu waliwaonyesha waandishi umahiri wao wa kuhifadhi Quraan, miongoni mwao ni wanafunzi wawili wenye umri wa miaka kati ya 8 na 10, Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan, na Ahmed Abdallah kutoka Bangladesh. Kijana mwingine aliyeonyesha ufundiwa kuhifadhi Quraan Tukufu ni Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia.
 Ahmed Abdallah kutoka Bangladesh
 Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia





No comments: