Na Abdulaziz Video,Lindi
Madiwani
wa Halmashauri za Wilaya ya Kilwa na Ruangwa Mkoani Lindi Zimeanza
Utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini
ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) kwa
Kupatiwa Mafunzo ya Siku 4 na Kuratibiwa na Tamisemi
Kuanza
kwa Hatua Hiyo kunafuatia kumalizika kwa Mafunzo kwa Watendaji wa
Halmshauri 6 Za Mkoa wa Lindi juu ya Namna ya Kushiriki na Kutekeleza
Mradi huo Utakaotekelezwa kwa Kipindi cha Miaka 5 Ijayo
Akifungua
Mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amezitaka Halmashauri
Hizo Kufuatilia kwa Umakini Mafunzo yanayotolewa na wakufunzi wa Chuo
cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo ili Kupata Uelewa Juu ya
Uendeshaji wa Halmashauri
‘’
Madiwani ni kiungo muhimu baina ya serikali na watendaji wa serikali
madiwani Musipokuwa Vizuri Mtaburuzwa na Watendaji hususan katika
Utendaji na Utekelezaji wa Miradi hasa Ikiwa Diwani Una Tabia ya Kuomba
omba na Kukopa kwa Mkurugenzi au Mkuu wa Idara Lazima Mjipime Nyie Ndio
wamiliki wa Halmashauri au hamjijui?’’Alimalizia Zambi
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi Akilakiwa na Mbunge wa Jimbo la Kilwa
Kusini,Suleiman Bungara(BWEGE)Mara Baada ya kuwasili katika Ukumbi wa MM
Hotel Mjini Lindi kwa Ajili ya Ufunguzi wa Mafunzo Elekezi kwa Madiwani
Wa Halmashauri za Kilwa na Ruangwa ili Kuelewa Jinsi ya Kutekeleza
Mfumo ya PS 3.
Bw
Joel Shimba,Mshauri wa Utawala Bora PS3(Kushoto )Wakielekezana jambo na
bw Victor Msoma,Mshauri wa Fedha PS3(Kulia)Kuhusiana na Mafunzo ya
madiwani wa Kilwa na Ruangwa Huku Bi Nseya Kipilyango,Mshauri wa Mifumo
ya Tehama wa PS 3(Katikati)Akifuatilia kwa Umakini
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Akitoa Hotuba yake ya Ufunguzi ambapo Pia Aliwataka
Madiwani Kuacha Siasa katika Kutekeleza Maendeleo ya Halmashauri
zao,Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Mikoa Mradi wa Ps,Bw Conrad Mbuya
Madiwani wa Ruangwa Pamoja Na Mwandishi wa Vikao Vya Baraza la Madiwani Ruangwa,Bahati kasabano (Kulia)wakifuatilia mafunzo hayo
Afisa
Mshauri wa Masuala ya Utawala Bora PS3, Nazar Sola akitoa Elimu kwa
Madiwani juu ya Utekelezaji wa Mifumo ya Utendaji na Utoaji Huduma
Baadhi
ya madiwani na watendaji wa halmashauri za Kilwa na Ruangwa Mkoani
Lindi wakifuatilia jambo katika semina Elekezi ya Kujenga Uelewa kwa
Halmashauri kupitia Mradi kuimarisha Uwezo wa Kutoa Huduma kwa Jamii
Chini ya Utekelezaji wa Mradi wa PS3 Unaofadhiliwa na USAID
Lukelo
Mhenga Mhasibu Msaidizi(kushoto) pamoja na Fina Maziku wote wa PS 3
wakifuatilia mada katika mafunzoa Hayo ambapo Halmashauri za Wilaya zao
za Kilwa na Ruangwa zikiwa ni Halmashauri za Awali kati ya 6 za Mkoa Huo
Zilizoanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za
umma(PS3) katika sekta za afya, elimu na kilimo.
No comments:
Post a Comment