Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez Alvaro
(kulia) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) mara baada ya kufika Ofisini kwake
Bungeni Dodoma leo.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
(kulia) akizungumza na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania , Rodriguez Alvaro (kulia) mara baada ya mwakilishi huyo kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez Alvaro
(kulia) akimwonesha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) sehemu ya taarifa ya mwaka ya
utekelezaji wa programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini mara baada
ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez Alvaro
(kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa
programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kufika
Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.
Wabunge
Mhe. Margaret Sitta (Kushoto) na Mhe. Najma Murtaza Giga, Mwenyekiti wa
Bunge wakiwa katika picha ya pamoja kwenye rangi za Malengo Mapya ya
Maendeleo Endelevu 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu
mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo nchini iliyofanyika
Bungeni, Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini
Tanzania , Rodriguez Alvaro
(kulia) kwenye rangi za Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia
wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa
malengo hayo Bungeni Dodoma leo.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
akiwa ameshika mabango mawili yenye malengo mapya 2 ya Maendeleo
Endelevu kati ya 17 ya Umoja wa Mataifa yanayotakiwa kutekelezwa duniani
kote kuanzia mwaka huu hadi 2030.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(kushoto) katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini Tanzania , Rodriguez Alvaro
(kulia) wakiwa na mabango yenye Malengo Mapya 2 kati ya 17 ya dunia
wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa
malengo hayo Bungeni Dodoma leo.
Mbunge
wa Urambo Mhe. Margaret Sitta (Kushoto) na Mhe. Najma Murtaza Giga,
Mwenyekiti wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja kwenye rangi za
Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia wakati wa Semina ya
wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo nchini
iliyofanyika Bungeni, Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez Alvaro
akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati wa Semina Kuhusu Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo
mjini Dodoma leo.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
akizungumza na Wabunge wakati wa ufungunzi wa Semina kwa wabunge kuhusu
Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma leo.
Mabango yenye Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia.
Mtaalam
wa Masuala ya Uchumi kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa
(UNDP), Rodgers Dhliwayo akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuyafikia
Malengo Mapya 17 ya dunia wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu malengo
hayo mjini Dodoma.
Mtaalam
wa Masuala ya Uchumi kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa
(UNDP), Rodgers Dhliwayo akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuyafikia
Malengo Mapya 17 ya dunia wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu malengo
hayo mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.
Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kusimamia
vyema utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kwa kuhakikisha kuwa Serikali
inatekeleza mipango iliyojiwekea kwa wakati ili kuimarisha ustawi wa
wananchi wanaowawakilisha na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati
akifungua semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo
ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango
wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).
Dkt. Tulia amesema kuwa Wabunge wana jukumu
la kuzingatia malengo hayo na kuhakikisha yanatekelezwa kwa kuwa
mipango yote na mikakati ya maendeleo hupitia Bungeni hivyo hawana budi
kusimamia malengo hayo ipasavyo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
Akizungumza
wakati wa semina hiyo Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya
Tano chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli inafanya
kazi nzuri katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia
na kuwataka Wabunge kuwa mabalozi wazuri katika utekelezaji wa malengo
hayo.
Bw.
Rodriguez ameongeza kuwa ni muhimu sana kwa Wabunge kuweza kuyaelewa
malengo hayo ya Dunia ili waweze kufanikisha utekelezaji na ufuatiliaji
wake katika ngazi zote za Taifa.
Mwaka
2015 nchi 193 ikiwemo Tanzania zilikubaliana kwa pamoja kutekeleza
mkakati wa kumaliza umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na
kupigania haki na usawa. Katika kufanikisha hilo nchi hizo zilikubaliana
kupitisha Malengo Endelevu 17 ambayo ni Kutokomeza Umaskini, Kukomesha
Njaa, Afya Njema na Ustawi, Elimu Bora, Usawa wa Jinsia, Maji Salama na
Usafi, Nishati Mbadala kwa Gharama Nafuu, Kazi zenye Staha na Ukuzaji
Uchumi, Viwanda, Ubunifu na Miundombinu, Kupunguza Tofauti.
Malengo
mengine yaliyoafikiwa na nchi hizo ni Matumizi na Uzalishaji wenye
Uwajibikaji, Miji na Jamii Endelevu, Kuchukua Hatua dhidi ya Mabadiliko
ya Tabia Nchi, Kuendeleza Uhai katika Maji, Kulinda Uhai katika Ardhi,
Amani, Haki na Taasisi Madhubuti na Ushirikiano ili Kufanikisha Malengo.
Naye
Naibu Katibu Mtendaji Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Maduka Paul Kessy
amesema kuwa Tanzania imejipanga kutekeleza malengo hayo kwa ufanisi
ili kufikia azma ya kuiondoa nchi yetu miongoni mwa nchi maskini na
kuiwezesha kuwa nchi ya uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda.
“Utekelezaji
wa malengo haya utakwenda sanjari na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Miaka Mitano ambao msingi wake ni kuchochea mabadiliko ya
uchumi na maendeleo ya watu.” Alisema Kessy.
|
No comments:
Post a Comment