Sunday, June 12, 2016

KUMI WENGINE WAWA MAMILIONEA KATIKA DROO YA TATU YA PROMOSHENI YA TUSKER

 Ni wiki nne zimepita sasa na tayari washindi 20 wameshakabidhiwa vitita vyao kupitia promosheni inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti ijulikanayo kama Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini na kumi wengine  kumi wametajwa leo katika droo ya tatu ya promosheni hiyo inayofanyika kila wiki. Wiki mbili zilizopita tulishuhudia washindi kumi kila wiki kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiondoka na Million moja kila mmoja kupitia promosheni hiyo inayoendelea. Katika droo ya tatu iliyochezeshwa leo, ambako washindi wengine kumi walitangazwa. 

Katika droo hiyo iliyofanyika ITV na kushuhudiwa na maofisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya Kubahatisha na wakaguzi wa nje, walitangazwa washindi kumi ambao ni Julius Lucas, Damas Mathei, Dustan Mhina, Hussein Shaban kutoka Dar es Salaam, Teddy Tarimo kutoka Kilimanjaro, Mwahu Hamis - Arusha, Mary Steve na Marietha Thomas - Morogoro, Domino Juma Shinyanga pamoja na Edison Maxini kutoka Mwanza. 

Mbali na washindi wa pesa taslim, pia kuna washindi kibao waliojishindia bia za bure papo hapo tangu promosheni ilipoanza. Mpaka sasa tayari takribani bia za bure zaidi ya 3000 zimeshagawiwa kwa watumiaji wa bia ya Tusker na zawadi nyingine kibao kama vile tshirt na kofia.

Akizungumza wakati wa droo hiyo Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Maston alieleza kuwa, promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ bado inaendelea na tayari washindi wa droo ya kwanza na ya pili wameshakabidhiwa vitita vyao. “Kwa kweli promosheni inaendelea vyema kabisa na washindi wanaendelea kushinda kutoka kila pande za Tanzania ambako sasa watumuaji wa Tusker wanaendelea kujitokeza kwa wingi kabisa kushiriki promosheni hii. 

Hali hii inaendelea kutupa moyo na kuona kuwa wateja wetu wapo pamoja nasi kutupa sapoti. Leo tumeshuhudia wenyewe washindi kutoka karibu kanda zote nchi nzima Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro and Dar es Salaam. Tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa promosheni bado inaendelea na bado tuna mamilioni kwa ajili yao, tunaamini kuwa ndani ya wiki saba zilizobakia tutapata washindi wengine wapya watakaoshiriki.”

Naye mmoja wa washindi Mary Steve kutoka Morogoro aliishukuru sana Kampuni ya Bia ya Serengeti kwani ilikua kama miujiza kwake kupata kiasi hicho cha pesa kwa kipindi hiki. “Nipata taarifa kuhusu promosheni hii kupitia maonesho ya barabarani nami kama mtumiaji mzuri wa Tusker nikaona nijaribu. 

Sikutegemea kama naweza kuwa kati ya wale wenye bahati, nilikua na shida sana na pesa kwa ajili ya kuongeza mtaji katika biashara yangu sasa naona Tusker imeniokoa na kutatua tatizo langu, nimepata pesa ya kufanyia biashara zangu nawashukuru sana. Ntaendelea kushiriki mara nyingi maana huwezi jua nikawa mshindi tena kwa mara nyingine.” Aliendelea kwa kuipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuendesha promosheni kama hiyo inayogusa maisha ya wateja wake kwa kubadili sehemu au maisha yote kwa ujumla. 

Washindi wote waliotangazwa leo watakabidhiwa vitata vyao katika hafla fupi zitakazofanyika sehemu mbalimbali wiki ijayo.


Afisa Mwandamizi wa ukaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tanzania ,Emmanuel Ndaki akihakiki taarifa za mmoja wa washindi waliotangazwa katika droo ya tatu,kushoto kwake ni meneja wa bia ya tusker Jasper Maston.Meneja wa bia ya tusker Jasper Maston akitoa maelezo kuhusu promosheni ya millioni mia moja na tusker fanya kweli uwini katika droo ya tatu iliyofanyika jijini dar es salaam mwishoni mwa wiki.
droo ikichezeshwa kupata washindi kumi wa tusker fanya kweli uwini. 


No comments: