Tuesday, June 21, 2016

KIKUNDI CHA UPENDO WOMEN'S GROUP CHA UBELGIJI CHATOA SHUKRANI KWA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI

Baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe za umoja wa kikundi cha kina mama wenye makazi nchini Ubelgiji kijulikanacho kwa jina la Upendo Women's Group.Kina mama wa Upendo wanatoa shukrani kwa kina mmoja aliyeshiriki katika hafla yao ya uchangishaji wa fedha za kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,sherehe hizi zilifanyika nchini Ubelgiji. 
Dr.Pendo Maro ambaye ndiye alikuwa mshehereshaji wa hafla ya uchangishaji wa fedha kwa kikundi cha kina mama cha Upendo Women's Group nchini Ublgiji akifungua uchangishaji wa sherehe hizo 
Rais wa kikundi cha Upendo Women's Group ambaye pia ndiye mwenyekiti cha kikundi hicho Mh:Theresia Greca,ametoa shukrani za dhati kabisa kwa Rais mstaafu wa Tanzania Mh: Benjamin William Mkapa kwa kuwachangia kikundi chao,Shukrani za pekee kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa mchango wao mkubwa wa kufanikisha zoezi zima la ufanikishaji wa fedha za kuisaidia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.{picha na maelezo toka Maganga One Blog} 
Pichani wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria sherehe za uchangishaji wa fedha kwa ajili ya hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Shukrani zinatolewa na wana Upendo Women's Group kwa ufanikishaji wa zoezi zima 
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Upendo Women's Group,kina mama wenye makazi yao nchini Ubegiji wametoa shukrani zao za dhati kabisaa kwa kila mmoja alishiriki vyema katika kufanikisha shughuli yao ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Wana Upendo wanapeleka shukrani zao kwa Rais Mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa kujitolea mchango wake,Bila kusahau shukrani zao kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima wa Tanzania nchini Ubelgiji.Wanatoa shukrani kwa vikundi mbalimbali vya maonyesho na kila mmoja aliyefanikisha zoezi zima. 
Katika kuchangisha fedha ili kusaidia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania, Upendo Women's Group waliaanda maonyesho mbalimbali ikiwemo na maonyesho ya mavazi.
Afisa Ubalozi Mr.Shayo {kushoto} pia nae alishiriki katika sherehe hizi fupi za uchangishaji wa pesa wa kuisaidia hospital ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Wana Upendo Group wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki na mchango wao mkubwa waliojitolea wa maafisa ubalozi wa Tanzania katika kufanikisha zoezi zima. 
Mmoja wa wageni ambaye siku hiyo alinunua bidhaa nyingi kutoka Tanzania ikiwa ni moja ya kuchangia wakina wa Upendo Women's Group ambao walifanya sherehe ya mfuko wa uchangishiaji hospital ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,kina mama wa Upendo wanatoa shukrani zao za dhati kwa kila mmoja aliyewezesha ufanikishaji wa Harambee hiyo.
Mmoja wa wageni waalikwa ambaye alichangia Harambee siku hiyo kwa kununua Kahawa halisi kutoka Tanzania.Wana Upendo wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki wa wageni hao.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mrs Agnes Kayola akielezea ushiriki wa serikali katika kuisaidia jamii na wananchi wake katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya.Kaimu huyo alikisifia kikundi cha kinamama wa Upendo Women's Group cha nchini Ubelgiji kwa jitihada wanazofanya kuisaidia hosptali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam. Wana Upendo Women's Group wanatoa shukrani zao za dhati kwa msaada waliopata kutoka kwa kaimu Balozi Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa ushiriki wao,shukrani zingine kwa Rais mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa mchango wake wa kukisaidia kikundi. 

No comments: