Saturday, June 4, 2016

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAENDESHA DROO YA PILI YA MILLIONI 100 NA TUSKER FANYA KWELI NA UWINI


Kundi la pili la washindi wa mamilioni ya Tusker watangazwa.
Wiki iliyopita ilishuhudiwa washindi kumi kutoka mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Kilimanjaro wakiondoka na Million moja kila mmoja kupitia promosheni inayoendelea ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli na Uwiniinayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti. 

Katika droo ya pili iliyochezeshwa leo, washindi wengine kumi walitangazwa. Katika droo hiyo iliyofanyika ITV na kushuhudiwa na maofisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya Kubahatisha walitangazwa washindi kumi ambao ni Rose Mkwizu, Sijali Ally, Anna Lazaro kutoka Dar es Salaam, Elizabert Wiliam kutoka Mlandizi –Pwani, Josephat Lukindo,George Mlay kutoka Kilimanjaro,Geofrey Manangwa kutoka Tanga, Wanzagi na Lucas Fransis kutoka Mwanza na Umoja Nyakwa kutoka Morogoro. 

Mbali na washindi hao ambao walijipatia zawadi ya pesa taslim, pia kuna washindi kibao waliojishindia bia za bure tangu promosheni ilipoanza. Bado kuna wiki nane ambapo zimebaki Millioni 80 kushindaniwa kwa kipindi hicho kilichobaki cha promosheni hiyo.

Naye mmoja wa washindi Elizabert Wiliam alisema kuwa Shoo ya kwanza iliyorushwa kupitia runinga ya ITV ndiyo iliyomsukuma kushiriki promosheni hiyo. “Nilitazama droo ya kwanza wiki iliyopita na siku zote mimi ni mtumiaji mzuri wa bia ya Tusker, baada ya muda punde tu nilienda kunywa huku nikiwa na shauku ya kushinda tu na kuingia kwenye droo” alisema bi Elizabeth. Aliendelea kwa kuipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuendesha promosheni kama hiyo inayogusa maisha ya wateja wao kwa kubadili sehemu au maisha yote kwa ujumla. Aliongeza kuwa pesa aliyoipata ataitumia katika kukuza biashara zake.

Naye Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela alieleza kuwa, promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ inaendelea vyema kabisa na washindi wanaendelea kushinda kutoka kila pande za Tannzania ambako sasa mikoa ya kanda ya ziwa imeungana nasi katika promosheni hii wiki iliyopita. Tuna washindi kutoka nchi nzima, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Dar es Salaam. 

Tunapenda kuwathibitishia wateja wetu kuwa promosheni hii si ya watumiaji wa bia ya Tusker waliopo Dar es Salaam tu bali kwa ushahidi huu wa washindi kutoka mikoa mingine unatosha kuthibitisha kuwa ni ya nchi nzima.

Washindi wetu wa wiki iliyopita watapokea zawadi zao za fedha taslim Million 1 katika hafla fupi ya makabidhiano itakayofanyika leo jijini Dar es Salaam na Moshi.
Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akiokota vocha ya ushindi katika droo ya pili ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua akitazama kwa makini mchakato mzima, anayefuata ni muongozaji wa shoo hiyo Abdallah Mwaipaya ambaye pia ni mtangazaji wa ITV
Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kulia) akimkabidhi vocha ya mshindi afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua ili kuhakiki taarifa za mshindi wakati wa droo ya pili ya promosheni ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kulia) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini wakati wa droo hiyo, pembeni yake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua akifurahia jambo alilosikia kutoka kwa mmoja ya washindi kupitia njia ya simu.

No comments: