KATIKA harakati za kuhabarisha jamii kwa maranyingine EFM redio imeleta mapinduzi kwa kufanya vipindi vyote moja kwa moja kutoka mtaani kwako leo, kuanzia kipindi cha Joto la asubuhi kinachorushwa kuanzia saa 12:00 - hadi Saa 3:00 asubuhi, pamoja na vipindi vyote kama sports .
Headquarters, Uhondo, Ladha 3600, na kumalizia na kipindi cha Ubaonikwa kushirikisha wakazi wa mtaa husika pamoja na kujadili mambo kadha wa kadha kuhusiana na kero, changamoto, kwa lengo la kuwaleta karibu wasikilizaji wake.
Mbali na vipindi hivyo pia kuna burudani kutoka kwa wasanii wa singeli kama M-cizo, Young Yuda, Majid Migoma, Easy Man, pamoja na Sholo Mwamba.
Wakazi wa wilaya ya Temeke wakisikiliza matangazo ya moja kwa moja katika viwanja hivyo vya mwembeyanga-Tandika.
Matangazo yalianza moja kwa moja katika kipindi cha joto la asubuhi kushoto ni Gerald Hando, Adela Tillya pamoja na Paul James (PJ).
Msanii wa singeli M- cizo akiwaburudisha wasikilizaji pamoja na watangazaji katika kipindi cha Joto la Asubuhi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Diwani Isaya Charles Mwita akitolea ufafanuzi changamoto zinazoikabili manispaa ya Temeke.
Watangazaji wa kipindi cha Sports Headquarters Kutoka kushoto ni Ibrahim Masoud (Maestro), Maulid Kitenge , Omari Katanga, wengine ni Musa Mwakisu, Yusuphu Mkule pamoja na Osca Oscar.
Wasikilizaji waliohudhuria katika eneo hilo wakijadili jambo na mmoja wa watangazaji wa Sport Headquarters Ibrahim Masoud (Maestro).
No comments:
Post a Comment