Thursday, June 2, 2016

DIWANI KATA YA CHANG'OMBE AFANYA ZIARA KEKO FURNITURE.


Mwakilishi wa wafanyabiashara Keko, Samuel kushaba akiwaonesha waratibu wa maendeleo maeneo wanayofanyia kazi ambapo amelalamikia gharama ziazowakabili kwa kuweza kukodi maeneo takribani matatu na yote wanayalipia kwa hela nyingi.

 Diwani wa kata ya Chang'ombe,Benjamini Ndalichako (Katikati) akiwa katika ziara ya upekuzi yakinifu katika maeneo ya biashara ya Keko na kuangalia changamoto zinazowakabili wafanyabioshara hao.
Diwani kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake na kueleza changamoto alizoziona na kusema atalifanyia kazi kwa kushirikiana na waratibu wa maemdeleo Manispaa ya Temeke na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wenye eneo kubwa ambalo wanahitaji kufanya uwekezaji wa kujenga maeneo ya biashara na kuwakodisha.
Haya ni mazungira hatarishi yakiwa katikati ya wafanyabishara wa eneo la Keko Furniture ambalo yanaweza kuwa chanzo cha mlipuko wa magonjwa kwa wafanyabishara na wakazi wa eneo hilo.

Na Zainab Nyamka,Blogu ya Jamii.
DIWANI wa Kata ya Chang'ombe Benjamin Ndalichako amefanya ziara katika maeneo ya biashara samani za ndani maeneo Keko Furniture na kujionea mazingira hatarishi wanayofanyia kazi na kuweka mikakati ya kuwasaidia wafanyabishara hao akishirikiana na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo wanakadiriwa kuwa na eneo kubwa sana ambalo wanaweza kuwekeza kwa kujenga maeneo yatakayotumika kwa ajili yao.

Ndalichako akiwa ameambatana na baadhi wa wajumbe wanaoratibu maendeleo wilaya na kujionea mazingira wanayofanyia kazi wafanyabiashara hao huku baadhi yao wakiwa hawalipi kodi. Amesema lengo kuu la ziara hiyo ni upekuzi yakinifu  ambapo wameona  vitu vingi sana ikiwemo mazingira hatarishi hasa ukizingatia hawana vifaa vya kujikinga na ajali pamoja na maradhi ikiwemo kifua kutokana na vumbi la mbao pale wanaporanda.

"Mazingira wanayofanyia kazi ni hatarishi na tumeona kwahiyo tunayemuwakilishi wa Salvatory Hinjo na ameahidi kulishughulikia hilo kwa kupeleka kwa mtendaji mkuu kwani wana eneo kubwa sana wanaweza kuwekeza kwa kujenga majengo watakayofanyia biashara,"amesema Ndalichako.

Kutokana na hali aliyoiona Ndalichako ameamua kukaa na wafanyabishara wa eneo hilo na kuzungumzia mazingira hatarishi pamoja na mgogoro uliopo baina ya NHC na wafanyabiashara ambao wamepewa taarifa ya awali ya kuhama kwenye maeneo yao na kuweka msimamo kuwa limeshafika mkononi mwake na atalishughulikia.

Naye mwakilishi wa wafanyabiashara wa Keko Samuel Kashaba  amesema wanachokiomba ni kupatiwa maeneo hayo na sio watakapojenga wapewe watu wengine wakati wao wapo siku nyingi na hata kabla ya kuhamishwa wapatiwa sehemu ambayo watahamishia kazi zao. Hata hivyo amelalamikia mazingira wanayofanyia kazi na kusema hawana budi kukodi maeneo matatu tofauti na gharama zinazidi kuwa nyingi kwa upande wao.

No comments: