Tuesday, June 28, 2016

WANAHABARI WATEMBELEA VIJIJI VINAVYO PAKANA NA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE

Baadhi ya Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale inayosifika kwa uwepo wa Sokwe Mtu.
Usafiri unaotegemewa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ni Boti na Mitumbwi .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,Pascal Shelutete (Mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda wakielekea katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi hiyo,Wengine ni wmwandishi wa gazeti la Uhuru,Jackline Massano na kulia ni Mhariri wa gazeti la Jamhuri ,Mkinga Mkinga.
Wanahabari ,Said Mnekano maarufu kama Bonge wa Clouds fm,aliyesimama nyuma.akiwa na Asiraji Mvungi pamoja na muongoza watalii ,Rashid Omary wakiwa katika moja ya boti zinazotumika kama njia ya usafiri katika Hifadhi ya  Taifa ya Mahale.
Waandishi ,Beatrice Shayo na Nora Damian wakijaribu kushuka kutoka katika boti.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akionozana na wanahabari kutembelea kijiji cha Nkokwa kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.
Ili kuwafikia wananchi maeneo mengine wanahabari walilazimika kuvua viatu na kupita katika maji.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAP A) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nkonkwa wilayani Uvinza.
Baadhi ya wananchi wanaounda vikundi vya wajasilaimali wakimsikiliza Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete (hayupo pichani ) alipoongozana a wanahabari kutembelea vijiji vinavypakana na Hifadhi ya Taifa ya Miima ya Mahale.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,MhifadhiRomanus Mkonda akizungungmza katika kikao hicho.
Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja akijaribu kusukuma chombo chake kwa kutumia kandambili wakati akisafiri katika ziwa Tanganyika.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale,Romanus Mkonda akitoa maelezo mafupi mbele tya waandishi wa habari waliotembelea vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo iliyopo mkoani Kigoma.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda akizungumza na wananchama wa vikundi vya kijasiliamali vinavyojulikana kama COCOBA vinavyosaidiwa na hifadhi hiyo (hawapo pichani.
Baadhi ya wanachama wa vikundi wakiwa katika mkutano na watumishi wa TANAPA pamoja na wanahabari waliotembelea vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza katika mkutano huo ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda.
Baadhi ya Wanahabari walioitembelea vijiji hivyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Katumbi ,Issa Zuber ,kijiji kimojawapo ambacho wanachi wananufaika na msaada wa mafunzo ya ujasiliamali unaotolewa na TANAPA,
Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano ,Juma Makumbi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Pascal Shelutete mara baada ya kuzungumza na wanachama wa vikundi vinavyopewa msaada na shirika hilo .

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.
Wananchi   wa  vijiji vya  Buhungu  na  Konkwa  vilivyoko  mwambao mwa   ziwa Tanganyika   wilaya   Uvinza  mkoani  Kigoma  wanalazimika   kuhifadhi  mamilioni  ya  fedha  za  miradi   ya  vikundi  vyao   kwenye  masanduku   ya  chuma  na  kuyafukia  chini   ya  ardhi   kutokana  na  ukosefu   wa  huduma  za taasisi  za  fedha  utaratibu  waliodai   kuwa  unaotishia  usalama  wa  fedha  hizo  na  pia  maisha  yao .

Wananchi hao  pamoja   na  kuwashukuru   wadau   wanaowasaidia  likiwemo  Shirika  la  Hifadhi za Taifa  Tanzania (TANAPA) kupitia  Hifadhi  yake  ya  Milima ya Mahale  wamesema wanatumia  njia  hiyo  kutokana  na  kuogopa  kusafirisha  kiasi  kikubwa  cha  fedha  umbali  mrefu  ili   kuzifikia  taasisi  za  fedha  zilizoko  kigoma  mjini  na wameiomba  serikali   na  asasi  za  fedha  kusogeza  huduma  katika  maeneo  ya vijijini.

Mkufunzi mkuu wa vikundi vya benki ya jamii ya uhifadhi (COCOBA) vinavyo fadhiliwa na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA), Simada Andrea amesema  kuwa vikundi hivyo vinavyoizunguka hifadhi ya milima ya mahale, vina sifa za kupewa mikopo lakini benki zimekuwa zikiwakataa na kuwapa masharti magumu.

“Sifa za kupewa mikopo wanazo…tatizo benki zinakataa kuwakopesha kwa sababu ya umbali, zinawataka watu wa mijini kwa madai kuwa wataweza kuwafuatilia,” alisema.

Alisema vikundi hivyo, vimesajiliwa na serikali za vijiji na halmashauri ya wilaya ya uvinza iliwahi kuvikopesha kwa majaribio sh. milioni 3 na vikarudisha kwa wakati.

“Naomba niziambie benki kuwa vikundi vya cocoba vinakopesheka na vinalipa kwa wakati,” alisema.
Hata hivyo, Andrea aliziomba taasisi hizo za kifedha kupeleka huduma katika maeneo yao ili ziwawezeshe kufanya shughuli zao kwa urahisi na kwa uhuru hatua itakayowaongezea tija na ufanisi.

Naye, afisa mtendaji wa kijiji cha Nkonkwa, Issa Fungameza alisema kuna vikundi hivyo kwa sasa vinatunza fedha zao katika kiboksi cha chuma kutokana na benki kuwa mbali.

“Vikundi vinakopesheka, kwa kuwa benki ziko mbali hivyo wanashindwa kupeleka fedha hizo benki na kuamua kuzitunza kwenye kiboksi cha chuma,” alisema.

fungameza aliiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa undani zaidi kwa kuvikopessha vikundi hivyo ili viweze kujiinua kiuchumi na kimaendeleo.

Mkuu wa idara ya ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Mahale,Romanus Mkonda alisema TANAPA  imetoa  zaidi   ya  milioni   600  kuvisaidia  vikundi  zaidi  ya  70  vya  wananchi  katika  vijiji  hivyo   kupata  mafunzo   ya   ujasiria mali ,  uhifadhi  wa  mazingira   na   mitaji,   hatua  inayolenga   kuwaepusha    wananchi  hao  kujihusisha  na    uharibifu  wa  mazingira  na  ujangili  katika  maeneo  yaliyohifadhiwa  ikiwemo  Hifadhi ya Taifa  ya  Milima  ya Mahale






No comments: