Thursday, June 9, 2016

Bayport yaendelea kutoa hati za viwanja kwa wateja wao

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, katikati akizungumza baada ya kumpa hati yake mteja wao wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Ibrahim D Mahinya. Kulia ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.


TAASISI ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mikopo imeendelea kugawa hati za viwanja kwa wateja wao walionunua viwanja katika mradi wao uliopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, uliozinduliwa rasmi mwezi Mei mwaka jana.


Wateja waliokabidhiwa hati zao ni pamoja na Ibrahim D Mahinya na Desdery Selestine Mkenda ambao wote kwa pamoja walikuwa miongoni mwa wateja waliojiunga na huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport.
Ibrahim Mahinya kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa hati ya kiwanja cha Vikuruti, kutoka Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mwenye miwani ni Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme na Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.


Akizungumza jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema kusudio lao ni kugawa hati kwa wateja wao mapema iwezekanavyo ili kujitofautisha na wadau wengine wanaojihusisha na mambo ya uuzaji wa ardhi kwa njia mbalimbali.


Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme katikati akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desdery Selestine Mkenda. Kulia ni Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.


Alisema kwamba hati zinazotoka kwa mwaka huu ni zile zinazohusu wateja walionunua viwanja hivyo katika mradi wa Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, mradi uliopokewa vizuri na Watanzania, jambo lililochangia Bayport kupanua wigo huo kwa kuanzisha miradi mingine ya Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa.

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani Ibrahim D Mahinya. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Mteja wa kiwanja cha Vikuruti vinavyotolewa na Bayport, Ibrahim D Mahinya akizungumza jambo.
Ibrahim Mahinya, akitia sahihi ya dole gumba kama njia ya kukamilisha utaratibu wa makabidhiano ya hati yake.

Thabit Mndeme katikati akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya hati za viwanja.
Mteja wa viwanja vya Vikuruti, Desdery Mkenda kushoto akishuhudia nyaraka zinazohusiana na mambo ya hati yake aliyokabidhiwa baada ya kuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kununua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Katikati ni Meneja Biashara wa Bayport, Thabit Mndeme na Afisa Sheria wa taasisi hiyo Mrisho Mohamed.

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kulia akipeana mkono wa na mteja wao Ibrahim Mahinya baada ya makabidhiano ya hati yake ya kiwanja cha Vikuruti kukamilika.


“Tumepania kuwa tofauti na wadau wengine wanaotoa huduma ya ardhi, kwa kuhakikisha mteja wetu anapata hati yake haraka na bila usumbufu wowote kwa ajili ya kumuondolea kero za ufuatiliaji wa hati.


“Tunawaomba Watanzania waendelee kuiunga mkono Bayport kwa kuchangamkia fursa za mikopo katika miradi yetu yote ukiwamo wa Chalinze, Kigamboni, Kilwa, Kibaha na Bagamoyo ambayo vinauzwa kwa mita moja ya mraba Sh 10,000 Bagamoyo, Chalinze Sh 4500, Kibaha Sh 9000, Kilwa Sh 2000 na Kigamboni Sh 10000,” Alisema Mndeme.

Naye Mahinya aliyekabidhiwa hati yake kutoka Bayport alisema kwamba amefurahishwa kupewa hati kwa haraka jambo ambalo ni tofauti na matarajio yake kutokana na suala hilo kuwa na mzunguuko mkubwa.

“Nimepata hati yangu kwa haraka mno, hii ni tofauti na matarajio yangu kwa sababu nafahamu suala la hati linavyokuwa na mkanganyiko mkubwa kwa sababu linashirikisha mikono ya watu wengi na lina mambo mengi pia, ila kwa Bayport kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo nalazimika kusema kuwa utaratibu wa kazi wa taasisi hii umenivutia,” Alisema.

Mteja mwingine Mkenda aliwashukuru Bayport kwa kumpatia hati yake, baada ya kuwa mmoja wa Watanzania aliyejipatia viwanja vya Vikuruti vilivyozinduliwa na taasisi hiyo mwaka jana mwezi wa tano, huku huduma hiyo ya viwanja ikipatikana katika ofisi zote za Bayport.


Mbali na mikopo ya viwanja, Bayport pia wanatoa huduma ya mikopo ya haraka ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa, huku mikopo hiyo ikiwa haina amana wala dhamana.

No comments: