Sunday, May 8, 2016

WANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI WAJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu (wa pili kushoto), akimkabidhi Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel, kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo kwa waimbaji wa nyimbo za injili uliofanyika Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima na Rais wa chama hicho, Ado Novemba.
Hapa mwimbaji nguli wa nyimbo za injili Mzee Kitenzogu Makassy akikabidhiwa kadi yake baada ya kujiunga na NHIF.
Burudani kutoka Kwaya ya Victorous Station ya Mwananyamala ikiendelea.
Wanakwaya wakibadilishana mawazo katika uzinduzi huo.
Burudani zikiendelea.
Waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Nabii Flora la Salasala wakitoa burudani.
Wanakwaya ya Ukombozi ya Kanisa la Anglikana Tegeta wakionesha umahiri wa kumtukuza mungu kwa kuimba.
Muonekano wa meza kuu katika uzinduzi huo.
Ushuhuda ukitolewa kuhusu mungu anavyowatendea watu wake miujuzi.
Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima (kushoto), akiwa ameketi na mgeni rasmi mama Joyce Hagu.
Maofisa wa NHIF kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa tayari kuwandikisha wanachama wapa katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Derick Ndyetabula, Margaret Malangalila na Dk.Fortunatus Salala.
Mchungaji David Nyanda ambaye ni muimbaji (wa pili kulia), akionesha manjonjo wakati akitoa burudani kwa kuimba katika uzinduzi huo.
Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Waimbaji na maofisa wa NHIF kutoka Kinondoni wakifuatilia uzinduzi huo.
Rais wa Chamuita, Ado Novemba akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Furaha na shangwe zikiendelea katika uzinduzi huo watu wote mikono juuu.
Meneja wa NHIF Wilaya ya Kinondoni, Constantine Makala akitoa darasa kuhusu faida za kujiunga na NHIF na jinsi ya kujiunga.
Dk.Fortunatus Salala wa NHIF akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili akielezea jinsi alivyonufaika na mfuko huo baada ya kujiunga miezi miwili iliyopita pamoja na mke wake.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu (kushoto), akionesha kadi za wanachama hao baada ya kuzizindua. Kulia ni Maadam Ruti Mwamfupe.

Na Dotto Mwaibale

WANACHAMA wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), wamejiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ili waweze kupata matibabi ya uhakika pindi watakapo umwa.

Katika hatua nyingine Mlezi wa chama hicho Askofu Rejoyce Ndalima amewataka waimbaji wa nyimbo za injili kujianzishia miradi mbalimbali itakayowaingizia kipato badala ya kutegemea uimbaji pekee na amewasihi wanamuziki hao kuachana na utamaduni wa kudurufu (kukopi) kazi za wenzao badala yake wawe wabunifu katika kutunga nyimbo zao.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Afya kwa wanachama wa chama hicho Dar es Salaam jana kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ndalima alisema kuokoka sio kuwa mjinga hivyo ni vyema kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo.

“Kuokoka sio kuwa mjinga kwani kuna fursa za biashara ambapo mnatakiwa kuonesha uwezo wenu wa kuzifanyia kazi ili muweze kujikwamua kiuchumi badala ya kung’ang’ania kazi moja tu ya uimbaji,” alisema Ndalima.

Askofu Ndalima aliwataka waimbaji hao wajiunge na bima ya afya kwani hakuna mtu atakayechangiwa tena pindi atakapoumwa na kama ni msaada mtu husika atasaidia katika masuala mengine.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Joyce Hagu kutoka, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo, alisema Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfuko wa wasanii kutokana na kutambua mchango wao katika jamii.

Hagu aliipongeza NHIF kwa kufikisha huduma hiyo kwa waimbaji hao kwani itawasaidia katika maisha yao hasa pale watakapohitaji kutibiwa katika Hospitali mbalimbali.

Meneja NHIF Wilaya ya Kinondoni, Constantine Makala alisema kuwa huduma hiyo watalipia 76800 kwa mwaka mzima.
Alisema watu wote waliojiunga na huduma hiyo wanaweza kupa matibabu katika Hospitali zilizoainishwa pamoja na kupata dawa katika maduka 200 yaliyosajiliwa na NHIF.

No comments: