Wednesday, May 4, 2016

WAFANYAKAZI WA CRDB TAWI LA MLIMANI CITY WATOA ELIMU KUHUSU 'INTERNET BANKING' KWA WATEJA WAKE.

BENKI ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wamewapa semina wateja wajasiliamali wa benki hiyo kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya Mtandao yaani Internet Banking. 

Huduma ya Internet Banking itawajengea uwezo wajasiliamali hao katika nyanja mbalimbali kama vile kuwalipa mshahara wafanyakazi wake, kuangalia jumala ya mapata waliyanayo kwenye akaunti yake pamoja na kuangali jinsi pesa ilivyowekwa na kutolewa katika akaunti yako kwa njia ya mtandao wa Interneti.
Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango akizungumza katika semina ya wajasiliamali wenye akaunti za benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa huduma mbadala za benki ya CRDB jijini Dar es Salaam, Dr. Joseph Witts akizungumza na wajasiliamali wenye akaunti kwenye benki ya CRDB katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Meneja huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ya kieletroniki, Mangire Kibanda akifafanua juu ya huduma ya Interneti banking kwa wajasiliamali wenye akaunti za benki ya CRDB jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Ubungo plaza.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa katika semina ya wajasiliamali wenye akaunti za Benki za CRDB.
Baadhi wajasiliamali wakimsikiliza Meneja huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ya kieletroniki, Mangire Kibanda katika semina iliyoandaliwa na wafanyakazi wa CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.

No comments: