Umoja wa wanawake Tanzania Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arusha mjini wamefanya uchaguzi ili kumpata mwenyekiti wa (UWT) katika wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa (UWT) Mkoani hapa Flora Lazaro Zelothe, amesema kuwa lengo la uchaguzi huo ni kumpata mwenyeketi wa umoja wa wanawake Wilaya ya Arusha mjini na kuongeza kuwa watu wenye maslahi binafsi hawawahitaji bali watu wenye mapenzi mema na umoja huo.
Flora amewataka wanawake kuacha makundi kwani yamekuwa yakiwatenganisha na hayana faida yeyote zaidi yakubomoa ,Bali wafanye kazi kwa bidii nakujituma kwa kushirikiana na viongozi wao,ili kuleta mafanikio katikaumoja huo.
Mary Kissaka baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Arusha Mjini.
Baada ya kutangangazwa kuwa mshindi kwa kura 319, Bi Mary Kissaka amewashukuru wanawake kwa kumchagua kwa kumpa kura za heshma,na ameahidi kwamba atawatumikia UWT.Kuanzia ngazi Tawi, Kata ,hadi Wilaya kwa kushirikiana na wanawake.
Ameongeza kuwa Aatafanya ziara kila tawi ,ili kufanya tathmini ya uhai ya wanachama, ili kila mwanachamaaweze kulipa ada ya mwaka kwa wakati, Pia amesema kwa ataanzisha miradi mbalimbali kwa kushirikiana na UWT.
Sambamba na hilo amewashauri wanawake wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zinapojitokeza kwani wanaweza, na amewataka kuzitumia nafasi hizo vizuri ili kuleta maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Shabani Mdoe Katibu Mwenezi Uvccm Arusha naye alialikwa katika uchaguzi huo akiteta jambo.
UWT Wilaya ya Arusha Mjini wakiwa katika ukumbi wa CCM mkoa wakisubiria kumchagua Mwenyekitiwa UWT Wilaya.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Mkoani Arusha (UWT) Flora Lazaro Zelothe.
Katibu wa Jumuiya wa wanawake Tanzania Mkoa wa Arusha (UWT) Bi Fatma Tsea.
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Ndugu Feruz Bano (ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo).
Mjumbe anayewakilisha Wazazi katika Jumuiya ya Wanawake Arusha (UWT) Phidesia Mwakitalima akifatilia uchaguzi kwa makini.
Viongozi wa CCM wilaya ya Arusha wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wilaya ya Arusha Mjini Ndugu Wilfred Soilel, anayefuata ni Ndugu Feruz Bano ambaye ni Katibu Katibu wa chama wilaya
Wanawake wakishangilia baada ya kumpata mwenyekiti wa kuiongoza UWT Wilaya ya Arusha Mjini.Habari picha na Woinde Shizza, Arusha.
No comments:
Post a Comment