KUELEKEA
maadhimisho ya hedhi salama itakayofanyika Mei 28 , Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA) imesema itaendelea kujenga mabweni na chemba za kuhifadhi
na kuchomea taulo za kike ili kuwafanya wanafunzi wa kike kusoma katika
mazingira mazuri.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi
Yombo iliyoko wilayani Ilala, Meneja Mawasliano na Uhusiano wa TEA,
Sylvia Lupembe alisema wanafunzi wa kike wamekuwa na wakati mgumu katika
masomo yako kutokana na hedhi.
“
Wanafunzi wa kike wanashindwa kuhudhuria masomo kwa zaidi ya siku 80
kwa mwaka jambo ambalo linarudisha maendeleo ya mazomo yao, kwa
kushirikina na wadu wa elimu tumeona tuangalie suala la kuwasaidia, hasa
wale alioko kwenye shule ambazo ni vigumu kufikia,” alisema.
Alisema
kwa mwaka huu wa fedha, TEA kwa kushirikiana na wadu wa elimu
wanakamilisha ujenzi wa mabweni 11 ya wanafunzi wa kike hapa nchini.
Lupembe
alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuwezesha kupatikana
na taulo hizo za kike sambamba na mchango wao katika ujenzi wa bweni
katika shule ya Sekondari Pangani ambalo limegharimu sh milioni 20.
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo
Christine Kasyupa, aliwashukuru TEA na benki ya CRDB kwa mchango wao
ambao wamekuwa wkaiutoa katika shule hiyo kwani awali walishopokea
dawati.
Naye
Mwanafunzi Monica Singano anayesomba darasa la Saba A katika shule ya
msingi Yombo, alisema msaada huyo umekuja wakati mzuri hasa kutokana na
wanafunzi wengi kutoka kwenye familia mabazo hazina uwezo wa kugharamia
kununua taulo za kike.
“
Wengi wa wanafunzi hapa wanatoka familia zisionauwezo wa kununua taulo
za kike, wengi wanatumia vitambaa ambavyo haviwezi kuwafanya wanafunzi
kukaa shule kuanzia asubuhi hadi mchana, hivyo kulazimika kwenda
kubadili huku masomo yakiwa wanaendelea,” alisema
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa wakati wa hafla ya
kukabidhiwa vifaa vya kujihifadhi wanawake vilivyotolewa na Benki ya
CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya wanafunzi wa
shule hiyo. Kushoto ni Ofisa wa TEA, Happines Tandari, Ofisa Mawasiliano
na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad na
Mwalimu Emily Salumu. (Picha na Francis Dande)
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiimbo nyimbo katika hafla hiyo.
Ofisa wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Happines Tandari akizungumza kaba la makabidhiano ya vifaa hivyo.
Ofisa
Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia
Hassad (kushoto), akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo,
Christina Kasyupa (katikati) na mwalimu Salumu sehemu ya msaada wa vifaa
vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB
kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia
Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo,
Monica Singano sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake
‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu
Tanzania. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa.
Ofisa
Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia
Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo,
Sabina Yona, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo
za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu
Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa.
Ofisa
Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia
Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Amina
Abdalah, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za
kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu Emily
Salumu.
Ofisa
Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia
Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo,
Rehema Baina, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo
za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu
Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu
Emily Salumu.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiwa wamenyanyua juu maboksi
yaliyokuwa na vifaa vya kujihifadhi wanawake 'Taulo za kike'baada ya
kukabidhiwa na Benki ya CRDB kupitia TEA.
Wanafunzi wakiwa na furaha.
Maofisa wa TEA wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo.
No comments:
Post a Comment