Tuesday, May 10, 2016

TANZANIA YAFUNGUA OFISI YA KONSELI YA HESHIMA JIJINI TORONTO, CANADA

Aprili 29, 2016 Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya Heshima jijini Toronto, Canada. Mkataba huo ulitiwa saini kati ya Konseli wa Heshima, Bw. Deepak Ruparell na Mhe. Jack Mugendi Zoka Balozi wa Tanzania Nchini Canada ambaye aliiwakilisha Serikali ya Tanzania. Tukio hilo lilifanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo jijini Ottawa nchini Canada.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada akimkaribisha Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell kwenye chumba cha wageni cha Ubalozi mara baada ya kuwasili.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell (kushoto) na Bw. Adtya Jha (kulia), Mjumbe wa National Capital Commission, Ottawa ambaye alifuatana na Konseli wa Heshima Mteule.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada (mwenye tai ya Bendera ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell (kulia kwa Balozi), akifuatiwa na Bw. Richard Masalu, Afisa wa Ubalozi na mwisho, kushoto ni Bw. Leonce Bilauri, Mkuu wa Utawala Ubalozini. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Bibi Aziza Bukuku akifuatiwa na Bw. Paul Makelele ambao ni maafisa wa Ubalozi.
Tukio la kutiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya Heshima jijini Toronto, Canada likifanyika kati ya Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Tanzania nchini Canada ambaye anaiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell , likishuhudiwa na maafisa wa Ubalozi.
Baada ya tukio la kutiliana saini mkataba, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka na Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell , wanaonekana wakibadilishana nyaraka za tukio hilo.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada anaonekana akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell picha ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada akimpa maelezo Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell na hatimaye kumkabidhi Nembo na Bendera ya Taifa kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell nakala ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1963 kuhusu Utendaji wa Shughuli za Kidiplomasia na Taratibu za Kikonseli ikiwa ni moja ya vitendea kazi muhimu kwa matumizi ya ofisi.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada (mwenye tai ya Bendera ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell (kulia kwa Balozi) pamoja na wafanyakazi wote wa Ubalozi mara baada ya kuhitimisha tukio la kutiliamna saini mkataba.

No comments: