Thursday, May 26, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Baraza la viongozi wa dini mbalimbali kwa ujenzi wa amani nchini limezindua mtaala wa amani nchini utakao tumika kufundishia somo la amani katika shule za msingi.https://youtu.be/CqvJuoEpNYI

SIMU.TV: Watumishi wa afya nchini wameaaswa kuacha tabia ya kuiba dawa na kuziuza aidha kwa wagonjwa au maduka binafsi na kusababisha wagonjwa kukosa dawa pale wanapozihitaji. https://youtu.be/TUI7bnG49iQ

SIMU.TV: Afisa afya wa wilaya ya Geita amenusurika kupigwa na wananchi waliokua wanatakiwa kufanyiwa usaili kwa ajili ya zoezi la unyunyuziaji wa dawa majumbani kutokana na zoezi hilo la usahili kugubikwa na vitendo vya rushwa.https://youtu.be/Z2hPerqgOAo

SIMU.TV: Zaidi ya wanawake kumi katika manispaa ya Kigoma Ujiji wamefanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kundi la vijana lijulikanalo kama Teleza ikiwemo kupigwa na kubakwa.https://youtu.be/rFF1_rXwglo

SIMU.TV: Kampuni ya bia TBL imesema licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia pato la taifa bado inakabiliwa changamoto ya soko kutokana na wananchi walio wengi kushindwa kumudu gharama ya bia badala yake wanatumia vileo vya kienyeji.https://youtu.be/GIqenm9E1A0

SIMU.TV: Benki ya CRDB imetajwa kuwa benki bora zaidi Afrika mashariki kwa kutoa huduma za kibenki kwa wateja wadogo huku mkurugenzi wake Dr Charles Kimei akitajwa kuwa mtu mwenye mafanikio zaidi katika kuendesha shughuli za kibenki.https://youtu.be/ra3Y1kwKiuQ

SIMU.TV: Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi limetakiwa kujitangaza zaidi ili liweze kujulikana zaidi kwa wananchi na kuelewa kuhusu huduma zake.https://youtu.be/xfx0HlXWu30

SIMU.TV: Mradi wa ufugaji wa vifaranga vya samaki unaotekelezwa na kikosi cha JKT katika mkoa wa Mara utasaidia kuongezeka kwa samaki katika ziwa Victoria kutokana na samaki wengi kutoweka kutokana na uvuvi haramu. https://youtu.be/-Dci2BUyP30

SIMU.TV: Tanzania imejitoa kwenye kuandaa mashindano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kama Kagame Cup kutokana na kubanwa na ratiba za mashindano mengine. https://youtu.be/wurzAaE_PmE

SIMU.TV: Baadhi ya wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga wameipongeza timu hiyo kutokana na juhudi ilizoonesha katika mchezo wake wa fainali za kombe la shirikisho la soka nchini ambapo timu ya Yanga ilitwaa kombe hilo. https://youtu.be/1Vs1vxTW3Ig

SIMU.TV: Michuano ya kombe la mkuuwa majeshi nchini yanayoendelea jijini Dar es Salaam yanaonekana kuwa na hamasa kubwa kutokana na kila timu kuonekana kuutafuta ushindi. https://youtu.be/c-umgOAFynI

SIMU.TV: Maandalizi ya pambano la ngumi kati ya Kosmas Cheka dhidi ya Miltoni kutoka Malawi yamekamilika. https://youtu.be/DLuUOgkKh-0

SIMU.TV: Timu ilioigiza utamaduni halisi wa watanzania imeibuka mshindi katika shindano la kuigiza tamaduni tofauti tofauti. https://youtu.be/3M161vNo6XA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na wanafunzi kutoka nchi zaidi ya kumi na tano duniani waliokuja kwa ajili ya tamasha la utamaduni lililoandaliwa na shule za Feza. https://youtu.be/CzioLho3yEA

SIMU.TV: Kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho amekubali kujiunga na timu ya Manchester united ya nchini Uingereza. https://youtu.be/K4N5_Ue8RSw

SIMU.TV: Rais Dr Magufuli amewataka wakandarasi wazawa kuweka maslahi ya nchi mbele katika utendaji kazi ili kuwezesha lengo la serikali kufikia nchi ya viwanda;https://youtu.be/mRLEDHHojh4

SIMU.TV: Vifaranga vya kuku zaidi ya 5000 vimekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere vikiingizwa nchini kutoka nchi za nje kinyume cha sheria;https://youtu.be/vZUzKf49zV8

SIMU.TV: Waziri wa elimu sayansi na teknolojia nchini Prof. Joyce Ndalichako amewasilisha bajeti ya wizara yake huku sekta ya sayansi na teknolojia ikipewa kipaumbele; https://youtu.be/8-N4j5fZAhE   

SIMU.TV: Serikali mkoani Tanga imesema haitosita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atayehusika na uvunjifu wa amani na usalama mkoani humo;https://youtu.be/lxVtfjZbLnY

SIMU.TV: Jamii ya Wahadzabe mkoani Arusha wameuomba mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kuwasaidia pesa na chakula ili kuondokana na maisha ya kula asali na nyama pori tu; https://youtu.be/8j8lI9_bVVM

SIMU.TV: Ndugu za watu waliokufa maji katika ajali ya meli ziwa nyasa mkoani Ruvuma wameishukuru serikali kwa jitihada ilizozifanya tokea siku ya ajali mpaka leo;https://youtu.be/C0xju8Zo1A0

SIMU.TV: Baraza la taifa la uwezeshaji NIC limeitaka mifuko ya uwezeshaji nchini kujitangaza ili wananchi waweze kuifahamu na kuitumia; https://youtu.be/aC_ZOC1kDUg

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo wa wazalishaji bora viwandani zitakazofanyika mwezi ujao; https://youtu.be/FB7KORu563Y

SIMU.TV: Kampuni ya bia nchini TBL imesema inakosa mapato ya karibu asilimia 30 kutokana na kupungua kwa wateja hivyo kufikiria kupunguza gharama za uzalishaji;https://youtu.be/bVwTK8pIzGU

SIMU.TV: Kampuni ya usambazaji wa vifaa na mitambo ya Jumbo imepanga kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari na wapiga picha ili kuendana na sayansi na teknolojia;https://youtu.be/RQXsnncUnGs

SIMU.TV: Maonyesho ya wafanyabishara wa Misri na Tanzania hususani kwa wafanyabiashara wa bidhaa za mipira na plastiki yanatarajia kuanza kesho jijini Dar es salaam; https://youtu.be/rANiB0NLnuA

SIMU.TV: Serikali imempa muda wa siku saba rais wa PST kujieleza kwanini asichukuliwe hatua kwa kosa la kuwachezesha watoto katika pambano la masumbwi;https://youtu.be/xcYArNWlNI4

SIMU.TV: Shirikisho la riadha nchini pamoja na benki ya Azania wamepanga kuanzisha mashindano ya riadha kwa watoto kuanzia juni 5 mwaka huu;https://youtu.be/niojVUAU5UU

SIMU.TV: Kampuni ya Global Publishers leo imetoa zawadi kwa washindi wa nyumba na pikipiki katika shindano la shinda nyumba lililoanzishwa na kampuni hiyo;https://youtu.be/bUBL5X1Kbzs

SIMU.TV: Mashirika na taasisi mbalimbali zimeombwa kujitokeza kusaidia michezo mbalimbali inayowahusu walemavu wa viungo mbalimbali;https://youtu.be/44p6AUq3Fm4

SIMU.TV: Kamati ya uchaguzi ya TFF imeanza kutoa fomu kwa wagombea wa ngazi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa timu ya Yanga; https://youtu.be/vmcUeIUUhTw

No comments: