Monday, May 16, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Naibu waziri wa TAMISEMI amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya mradi wa mabasi yaendayo kasi ili mradi huo uweze kunufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.https://youtu.be/4Yqjks8mshM

Sakata la padre wa Anglikana jijini Dar es Salaam kufukuzwa na Askofu mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya waumini wa kanisa la Anglikana Magomeni kutoa kiti cha Askofu katika kanisa hilo kwa kudai kuwa kakiuka maadili ya kanisa hilo. https://youtu.be/2vqRkUn8J44

Tafiti zinaonesha kwamba sababu kubwa ya magonjwa ya saratani kwa binadamu inatokana na kutumia vyakula vyenye chembechembe za miyonzi ya nyuklia.https://youtu.be/CUKJnp17Mgk

Klabu ya sanaa na michezo ya The Little Theater Club imefanya matembezi ya hisani yaliokua yamelenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuchangia mapambano ya saratani ya matiti. https://youtu.be/VS0-4jQVEwQ

Wafanya biashara wadogo wauzaji wa nyama katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam wamekutana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na uongozi wa benki ya DCB  ili kumueleza changamoto zinazowakabili za mikopo pamoja na hali ngumu ya maisha baada ya kufungwa kwa machinjio hayo kutokana hali ya uchafu.https://youtu.be/AMRNAlJ2ouQ

Wafanyabiashara wa mbogamboga katika makutano ya mtaa wa Zanaki na Libya jijini Dar es Salaam wamelalamikia uongozi wa mtaa kutokana na kuwataka waondoke eneo hilo bila kuwaeleza sehemu ya kwenda. https://youtu.be/Xind4cn-xyM

Takribani wanafunzi 2761 wanaosoma shule ya msingi Kiheba na shule ya msingi Kibirizi mkoani Kigoma wanakabiliwa na uchache wa matundu ya vyoo huku wakitumia pamoja na waalimu matundu machache walio nayo. https://youtu.be/XDEtvRLF_yc

Wazee wasiojiweza wanaoishi katika kambi ya Amani ilipo mjini Tabora wameiomba serikali kutekeleza sera ya matibabu bure kwa wazee na watoto ili waweze kutatua changamoto za matibabu zinazowakabili. https://youtu.be/6a1ZBmhNpjQ

Wanawake wengi nchini Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla wamekua wakinyanyaswa na kutopewa huduma inavyotakiwa katika jamii. https://youtu.be/JYb-b-A93zM

Mtoto mwenye umri wa miaka minne Christina Mbona anaomba msaada kwa serikali na wasamaria wema kwa ajili ya kwenda India kupata matibabu ya uvimbe uliomtokea eneo la usoni. https://youtu.be/BDkcW32w2oE

Klabu ya Simba leo imeonja furaha ya ushindi katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuifunga Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.https://youtu.be/o4wMy28gewE

Michuanio ya wazi ya gofu ilioandaliwa na chama cha gofu nchini imehitimishwa leo katika viwanja vya Lugalo huku ikiwa imekabiliwa na changamoto ya mvua.https://youtu.be/BMtkr7h19mM

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka kumi na saba imetoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya timu ya vijana ya Marekani kwenye mchezo wao wa kirafiki uliochezwa huko nchini India. https://youtu.be/kLWsPkwz3JM

Tanzania imelezwa kuwa ni nchi ya pili barani Afrika kwa utengenezaji wa filamu zinazopendwa ikitanguliwa na nchi ya Nigeria. https://youtu.be/biNyyIrIuFw

Liverpool wameshindwa kutamba katika mchezo wao wa kuhitimisha ligi kuu ya Uingereza wakati Arsenal wao wameendelea kung’ara. https://youtu.be/_LCgR_X6xwE

Serikali wilayani Arumeru mkoani Arusha imeombwa kufuta umiliki wa shamba la mmiliki mmoja na kuligawa kwao baada ya mwekezaji mmiliki kushindwa kuliendeleza;https://youtu.be/9mRxXzGcWJU

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amepiga marufuku kwa wazabuni wote wanaotengeneza madawati kwa kutumia mabaki ya mbao maarufu kama mabanzi;https://youtu.be/cObF94kvSJw

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea amewataka waratibu wa elimu wote wilayani humo kufanya kazi zao kwa weledi ili kuinua kiwango cha elimu wilaya humo;https://youtu.be/hNHPZpNXea4  

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wameombwa kuyatunza mabasi yaendayo kasi pamoja na miundombinu yake ili mradi huo uweze kuleta manufaa;https://youtu.be/AFh9DwnPAH4

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali ya Tanzania imeamua kupambana na rushwa ili kuweza kuwapatia maisha mazuri watanzania wote;https://youtu.be/clMQOP3bgaQ

Baadhi ya wajasiliamali wanaofanya shughuli zao katika machinjio ya Vingunguti iliyofungwa na serikali ili kupisha ukarabati wameiomba serikali kufungua haraka machinjio hayo kuwawezesha kuendelea na shughuli zao;https://youtu.be/Dw7cQkP9XGM   

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kigoma wamesifu tabia ya mawaziri nchini kutembelea miradi mbalimbali inayoendelea nchini kuwa inachangia wakandarasi kufanya kazi zao kwa kasi kubwa; https://youtu.be/c2xaYUEmdRE

Halmashauri ya manispaa ya Njombe unaendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya stendi ya mabasi wilayani humo; https://youtu.be/qzwwvxwqJxs
Wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge wametakiwa kuwa na mahusiano maalumu na waandishi wa habari ili kuwezesha kufikisha taarifa zao kwa wananchi na kwa wakati; https://youtu.be/jzKLZk976ew

Jukwaa la wakristo Tanzania mkoani mbeya wamefanya maombi maalumu kumuombea rais Magufuli na watendaji wake ili kuendelea kuliongoza taifa kwa amani na utulivu; https://youtu.be/nscPI8O9O9U

Timu ya soka ya Simba hatimaye yafufuka na kuifunga timu ya Mtibwa kwa bao 1-0 na kuendelea kubakia katika nafasi ya tatu; https://youtu.be/I8fKx_Gchaw

Mabingwa wa soka wa Tanzania bara timu ya soka ya Yanga wataondoka nchini hapo kesho kuelekea nchini Angola katika mechi ya marudiano na Sagrada Esperanca;https://youtu.be/5zj2xd_RIi4

Ligi ya taifa ya kikapun imemalizika leo jijini Dar es salaam huku timu iliyofanya vibaya zaidi katika mshindano hayo ikiwa ni Young Warriors kutoka mjini Morogoro;https://youtu.be/n6qwG5KwuGc

Mashindano ya golf ya Lugalo Open yamekamilika hii huku waandaaji wakiahidi kukuza na kuendeleza mchezo wa golf Tanzania; https://youtu.be/qyHwOfnwWwU

Hofu ya kuwepo kwa bomu katika majukwaa mawili ya uwanja wa Old Trafford imepelekea kuhairishwa  kwa mchezo kati ya Manchester United na AFC Bournemouth;https://youtu.be/E50E8VAnldw

No comments: