Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru
Halfan Mshiro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema
wakiokota baadhi ya uchafu katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa
Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta walipozuru kaburi hilo katika
kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni
mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi na
kulia ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
Mtoto
wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi (watatu
kulia) akiongoza dua ya kumuombea baba yake hayati sheikh Kaluta Amri
Abeid wakati ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo
Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kushoto mbele) akizungumza wakati
ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru
katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri
Abeid Kaluta kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro.
Katibu
Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa Dkt. Suleimani Sewangi (mwenye
miwani) akisoma tawasifu ya hayati Sheikh Kaluta Amri Abeid Kaluta
wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo
Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa Dkt. Suleimani Sewangi (mwenye
miwani) akisoma tawasifu ya hayati Sheikh Kaluta Amri Abeid Kaluta
wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo
Jijini Dar es Salaam.
Bw.
Kassim Amotile (mwenye miwani) akigani Shairi lililoandikwa na marehemu
Mathias Mnyampala mwaka 1964 wakati wa kifo cha hayati Sheikh Kaluta
Amri Abeid Kaluta na kulipa jina la Kifo cha Sheikh Abeid, Pengo kuu kwa
Taifa wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika
leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia
Mjema na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo Bibi Nuru
Halfan Mrisho.Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kulia) akiongoza msafara wa
ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuzuru
Kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid
Kaluta katika kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro na
kushoto ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
No comments:
Post a Comment