Manufaa yanayotokana na hifadhi za taifa na vivutio vya utalii hayatoshi tu kutumika kama nyenzo ya kupunguza vitendo vya ujangili na uvamizi katika maeneo yaliyotengwa na serikali ikiwa hakutakuwa na ushirikishwaji wa kutosha na wa moja kwa moja kwa wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka rasilimali hizo.
Pamoja na mchango mkubwa wa utalii katika uchumi taifa na kuwepo kwa manufaa kwa vijiji vinavyozunguka hifadhi za taifa na vitutio vingine vya utalii, jamii bado imeshindwa kuzitambua faida hizo ili kushiriki kikamilifu katika kupambana na ujangili na uvamizi holela wa maeneo hayo.
Je, jitihada zinazofanywa na serikali na wadau kutoa elimu kwa jamii na kuibua fursa muhimu katika sekta hii zinatosha?
Ili kujibu swali hilo Jukwaa linalohusu masuala ya Usimamizi Shirikishi wa jamii wa maliasili mnamo Mei 26, 2016 limewakutanisha wadau wa mazingira, maliasili na utalii kujadili mambo muhimu yanayoweza kuchangia katika kufungua milango ya fursa katika sekta ya wanayamapori.
Mratibu wa Jumuiko la Maliasi Tanzania (TNRM), Faustine Ninga akifafanua jambo wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa Jamii wa Maliasili lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam.
Demetrius Kweka kutoka Engility, (wasimamizi na waendeshaji wa mradi wa PROTECT), akizungumzia hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo
Wadau wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo
Afisa Utalii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wilfred Msemo akiwasilisha mada
Meneja Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Selous, akiwasilisha mada wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa Jamii wa Maliasili lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment