Saturday, May 21, 2016

SAGCOT IHEMI CLUSTER YAFANYA MKUTANO WAKE MKOANI NJOMBE

SAGCOT Kongai ya ihemi imefanya Mkutano wake wa tathmini wa yale walio kubaliana katika kukuza uhusiano kati ya sekta binafsi na seriakali katika kuendelaza uwekezaji. Mkutano huo wa siku 2 ulimalizika Njombe Mei 20, 2016. 

Uliudhuriwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza na wakuu wa wilaya za Ludewa, Wanging'ombe, Mufindi, Kilolo na Iringa Mjini uliandaliwa na kituo cha SAGCOT chini ya Mkurugenzi Mtedaji Geofrey Kilenga.

Kongai (CLUSTER) ya Ihemi walijadili masuala ya uzalishaji, usafirishaji, Usindikaji pamoja na utafiti katika kukuza uwekezaji na kipato cha wananchi. Sekta binafsi ilihudhuriwa na makampuni makubwa yanayo jihudisha na kilimo pamoja na ufugaji kama ASAS, Darsh INDUSTRIES (RED GOLD), muungano wa wafugaji Ngombe Njombe. Pia Bi Neema Mwingu kutoka World Bank alitoa mada yenye kuonyesha kuwa Benki ya Dunia imetenga kiasi cha dola za kimarekani Milion 70 kukuza sekta binafsi inayokua (SME) ili waweze kushirikiana na wewekezaji wakubwa katika mnyororo wa thamani.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Njombe akiwakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Anatoly Chonya alisema Mikoa ya Njombe na Iringa ndio mikoa ambayo ikifanya vizuri katika kilimo na ufugaji basi tanzania itakuwa imeongeza pato la taifa maradufu, aliwaomba SAGCOT kuhakikisha wanazidisha juhudi za kukuza kilimo katika mikoa hiyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisistiza suala la sekta binafsi kuhemshimu makubaliano ya awali hasa ya kunufaisha wanannchi walio wakuta, pia alichukizwa na mtindo wa makampuni hayo kuhamisha ulipaji wa kodi ya mapato kwenda Dar es salaam jambo ambalo linapunguza pato la mkoa kwa kiwango kikubwa.

Naye Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jolwika Kasunga akichangia alisema " wawekezaji wana kuwa karibu sana na serikali mwanzoni wakati wa kuhangaikia vibali wanapo fanikiwa wanapotea mpaka wapate shida ingine" .

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisisitiza suala la masoko na wawekezaji kupata social licence kutoka katika jamii kabla ya kuanza uwekezaji hili litapunguza sana migogoro isiyo kuwa ya lazima.

Katika mkutano huo pia Mkurugenzi wa Sagcot Catalyst Fund alisema lazima sasa wakulima wadogo wawe matajiri la msingi ni kuhakikisha fedha zote hizi zinawanyanyua na kuwafanya matajiri.
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akichangia mada katika Mkutano wa tathmini wa yale walio kubaliana katika kukuza uhusiano kati ya sekta binafsi na seriakali katika kuendelaza uwekezaji (SAGCOT Kongai ya ihemi) uliofanyika Mkoani Njombe.
Sehemu ya viongozi kutoka katika mikoa ya Njombe na Iringa wakisikiliza mada. Katikati ni Spika wa Bunge Mstaafu, Mama Anna Makinga.
Mkuu wa wilaya Ludewa, Anatory Choya akizungumza katika Mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela nae alipata wasaa wa kuchangia mada katika Mkutano huo.
Wadau wakisikiliza

Spika wa Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Mama Anna Makinda akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.
Mkuregenzi Mtendaji wa SAGCOT akitoa mada
Picha ya pamoja.

No comments: