Mwanachama
wa Jumuiya ya Waastafu wa Muungano akisoma risala kwa Wajumbe wa Mfuko
huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa
Jengo la Sanaa Rahaleo chini ya Ufadhili wa PSPF kwa Kutoa Elimu ya
Kujiunga na Mfuko huo kwa Hiari.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano wakisikiliza risala
ya Mkutanmo Mkuu wa Mwaka ikisomwa wakati wa mkutano huo.
Mgeni
rasmin wa Mkutano huo Mkuu wa Jumuiya ya Wastaafu Mhe Nassor Salum
Jaziri Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni akiwa na Viongozi wa Jumuiya
hiyo meza kuu.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wakifuatilia Mkutano huo Mkuu.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar Ndg Khamis
Rashid, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Mwakilishi wa
Jimbo la Rahaleo Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira kuufungua mkutano huo
Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Jengo Sanaa Rahaleo
Zanzibar.
Mwakilishi
wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira akitowa nasaha
zake kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano
Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano wakimsikiliza mgeni
rasmin akifungua mkutano huo na kutowa nasaha zake.
Makamu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Ndg Ramadhani Nzori, akizungumza kabla ya kumkaribisha Afisa wa Mfuko wa
Hifadhi wa PSPF kuzungumzia umuhimu wa kujichangia kwa hiari katika
Mfuko huo kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa
Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo
Zanzibar.
Afisa
wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF Ndg Mohammed Salum akitowa maelezo ya
manufaa ya Kujiunga na Uchangiaji wa Hiyari kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya
Muungano na faida zake kupitia Mfuko huo wakati wa Mkutano Mkuu wa
Jumuiya hiyo uliodhaminiwa na PSPF.
Afisa
wa Mfuko wa PSPF Ndg Mohammed Salum, akitowa Elimu ya Mfuko huo wa
Hiari kwa wanachama wake jinsi ya kuchangia na manufaa watakayopata
wakiwa Wanachama.
Wajumbe hao wakifuatilia elimu ikitolewa na Afisa wa Mfuko wa PSPF wakati wa mkutano wao mkuu.
Afisa
wa PSPF akisisitiza jambo wakati akitowa Elimu hiyo ya kujiunga na
Mfuko wa Hiari wa PSPF kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya
Wastaafu wa Jamuhuri ya Muunhgano wa Tanzania.
Wajumbe wakisoma vipeperushi vya maelezo ya Mfuko wa PSPF. Imetayarishwa na OthmanMapara. Zanzinews.com.Zanzibar.
No comments:
Post a Comment