Tuesday, May 31, 2016

MILLION 100 NA TUSKER FANYA KWELI UWINI YAZINDULIWA NDANI YA KANDA YA ZIWA

Kikundi cha TYT kikitoa burudani wakati uzinduzi wa promosheni ya Million 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini kanda ya ziwa uliofanyika jijini Mwanza -Cross Park Bar Igoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Kanda ya Ziwa wakicheza kufurahia uzinduzi wa Tusker Fanya Kweli Uwini jijini Mwanza.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Kanda ya Ziwa Patrick Kisaka akitoa maelezo ya promosheni hiyo kabla ya kuzindua rasmi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa promosheni ya Million 100 na tusker Fanya Kweli Uwini, iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Mwanza.

Baada ya kutikisa jiji la Dar es Salaam na manispaa ya Moshi leo Kampuni ya Bia ya Serengeti imeendelea kuwapa raha wateja wake kwa kuzindua promosheni ya Milioni 100 na Tusker- Fanya Kweli na Uwini Kanda ya ziwa ambapo Millioni 100 za Tusker Lager kushindaniwa. 

Uzinduzi huo uliofanyika jijini Mwanza Katika Bar ya Cross Park iliyopo Igoma wilayani Ilemela, ulipambwa na maonyesho ya barabarani ambapo msafara ulianzia Kiwanda cha Serengeti Igoma na kuishia Cross Pack Bar huku ukipokelewa na shamrashamra za aina mbalimbali.

 Promosheni hiyo itawapa fursa wateja kujishindia pesa taslimu Milioni 1 kwa washindi kumi (10) kila wiki kwa muda wa wiki kumi na kufanya jumla ya Milioni mia kushindaniwa na Zawadi za bia kibao. Promosheni hii ilizinduliwa rasmi na itaendeshwa kwa muda wa wiki kumi. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kampuni hiyo pamoja na wana habari.

 Hii si mara ya kwanza kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti kuendesha promosheni kama hii kwani ni wengi wameshanufaika kupitia promosheni mbalimbali za mfumo huu na hata kubadili maisha ya watumiaji wa bidhaa zake kwa kiasi kikubwa. Kupitia bia ya Tusker Lager Kampuni hiyo inaendeleza kile kilichokuwepo cha kurudisha fadhila na kutoa shukrani kwa watumiaji wa bia ya Tusker Lager.                  

Wateja wanaweza kujaribu mara nyingi kadiri wawezavyo. Ili kuwa mshindi wa Tusker milionea, washiriki wataingizwa moja kwa moja kwenye droo kutokana na vocha walizojaza mahali walipopatiwa huduma na wataweza kujishindia pesa taslimu na droo hizo zitachezeshwa kila wiki. 

Mtumiaji anapofungua bia ya Tusker Lager (500ml) chini ya kizibo anaweza kupata kizibo cha ‘Tusker Milionea’ hii itamuingiza katika droo ya kupata Milioni moja, au anaweza kupata ‘Bia ya Bure’ – hii inampa mteja bia ya Tusker papo hapo alipohudumiwa na ikiwa atapata ‘Jaribu tena’ utaendelea kuburudika kistaarabu ili kuongeza nafasi yako kuibuka mshindi. Promosheni hii itasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini ili kuleta ufanisi zaidi.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo jijini Mwanza Meneja Mauzo wa Kanda ya ziwa wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Patrick Kisaka, aliwashukuru wageni wote kwa kuja kuwaunga mkono na kusema kuwa uzinduzi wa promosheni hiyo  ni muendelezo wa kile kilichoanza wiki mbili zilizopita ikiwa ni kutoa shukrani kwa wateja wao kwa kusapoti bidhaa zao.

Alisema “kuendesha promosheni hii ni kurudisha shukrani kwa wajeta wetu kwa kutuunga mkono na kusapoti bidhaa zetu, ambapo tunampa mteja sehemu ya faida tuliyopata Katika mauzo yetu hivyo kuwapa wateja wetu wigo mpana wa kujiinua kimaisha. Kupitia bia yetu ya Tusker Lager tunampa fursa mnywaji na mdau wa bia hii kufanya kweli hivyo watumiaji wa bia ya Tusker wanaweza kujishindia shilingi Millioni moja kwa washindi kumi kwa muda wa wiki kumi ambao tutawapata kutokana na droo tutakazochezesha kila wiki.”

Naye ‘Commercial Planning & Activations Manager’ wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Denis Tairo alisema “Kanda ya ziwa ni sehemu muhimu sana kwa soko letu, wadau wa jiji hili la Mwanza mmekua mstari wa mbele na haikua rahisi sisi kufika hapa leo bila ninyi wadau wetu basi nasi tunasema burudika na bia ya Tusker ili upate nafasi ya kushiriki katika promosheni hii, haijalishi upo wapi na unafanya nini lakini amini kuwa kila wiki ni Millioni kumi zinatolewa kwa watumiaji kumi wa bia ya Tusker.”

Wapenzi na wadau wa Tusker wataweza kushuhudia droo za Promosheni ya Milioni 100 na Tusker zitakazofanyika kila wiki siku ya ijumaa na kurushwa moja kwa moja katika runinga.  Washindi watakaopatikana watakabidhiwa pesa zao ambazo watazipokea kwa njia ya mtandao kila ijumaa inayofuatia kwenye hafla maalum ya makabidhiano. Milioni 100 na Tusker Fanya kweli na Uwini itadumu kwa muda wa wiki kumi nchi nzima. 

No comments: