SERIKALI
ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria
kuwa Serikali ya mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.Rais
Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita
kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa
Viwanda.
Wakati
Serikali ikisisitiza kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti
kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono
hilo kila mmoja amekuwa na kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo
hilo.
Abdallah
Ulega ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani
Pwani kwa upande wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha
dhamira na kiu ya kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo
kuwa na viwanda.
Anasema
kuwa lazima wao kama wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge
wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi
haya kwani wameahidi hivyo lazima watende. Ulega anasema kuwa Jimbo la
Mkuranga ni kubwa na linarutuba ya kutosha hivyo anakaribisha wawekezaji
kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda vidogovidogo na vikubwa katika
kilimo hasa cha mazao mbalimbali Kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.
Anasema
kuwa kuna jitihada kama Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba
jimbo lake ni miongoni mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya
Serikali ya kutaka mageuzi ya viwanda. “Kimsingi jimbo langu la Mkuranga
ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo
maana naomba wahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda.”anasema ulega
Anasema
kuwa kutokana na utajili wa Ardhi yenye rutuba wanaweza kujenga viwanda
vya kusindika mazao lakini pia kwa sababu eneo lao ni kubwa basi hata
viwanda vya kubangua korosho na kujengwa Kwa viwanda hivyo kutasaidia
kuleta ajira katika eneo hilo.
Anasisitiza
kuwa ndio maana wakati akichangia mpango wa wa maendeleo wa Serikali
Kwa miaka mitano ameomba Serikali na wahisani kujitokeza Mkuranga lakini
Kwa upande wa Serikali kuiweka Mkuranga kuwa sehemu yenye hitaji la
ujenzi wa viwanda. Anasema amebainisha wazi kiu ya wananchi wa jimbo
lake la kutaka maendeleo na ajira hivyo bila kuwepo na viwanda hakuna
ajira inayoweza kuwepo na zaidi vijana watazidi kulaumu serikali yao.
“Nimesema
wazi kuwa Mkuranga kuna matatizo ya miundombinu mbalimbali ikiwamo
barabara.Maji .kilimo na mambo mengine na katika baadhi ya maeneo haya
nashukuru baadhi ya marafiki wameitikia mwito wangu na wameweza kusaidia
katika kichimba visima ambapo wananchi wangu wameaza kupata Maji safi
na salama.”anasema Ulega
Anasema
kuwa anawashukuru African Foundation Reflection Kwa kuonesha moyo wa
kusaidia na juhudi hizo zote zimetokana na jitihada zake za kutaka kuona
siku moja Mkuranga inakuwa ya kutolea mfano tofauti na ilivyo
sasa. Aidha katika mpango huo wa maendeleo Kwa miaka mitano Kwa Serikali
ameomba kujengewa barabara Kutoka Kisiju hadi Mkuranga Kwa kiwango cha
lami kwani barabara hiyo ni muhimu Kwa wananchi wa wilaya hiyo lakini
hata wale wanaotoka Mafia.
Pia
anasema katika mpango mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano
Kuhusu maendeleo ya miundombinu nchini na hapo aliangalia wilaya ya
Mafia kwa sababu pale kuna bandari na watu wake pia ndiyo wazalishaji
wakubwa wa korosho na samaki. Anasema kuwa pia kwenye kata yake ya mbezi
kwaniaba ya wananchi wake wa Mkuranga wangeishauri Serikali kuwa eneo
la viwanda ili wananchi wake wawe sehemu ya uzalishaji wake.
Aidha
Ulega anazungumzia suala la kuondoa kero ya uhaba wa upatikani wa Maji
katika jimbo hilo ambapo Serikali ingefanya bidii ya kutoa maji hayo
kutoka katika mto rufiji kupitia kibiti hadi kufika Mkuranga na hatimaye
Dar es Salaam.Anasema haiwezekani Kwa miaka nenda rudi tatizo la Maji
halipatiwi ufumbuzi wakati Mkuranga inapitiwa kwa karibu na Mto Rufiji
ambapo mikakati madhubuti ya kuleta Maji ikifanyika tatizo hilo litabaki
kuwa historia katika eneo hilo.
Anasema
tatizo la ajira Kwa vijana ni kubwa mno hivyo wanashukuru Serikali Kwa
kutambua umuhimu wa kutilia mkazo uazishwaji na ufufuaji wa viwanda
kwani eneo hilo ndilo linaweza kuwa.msaada Kwa vijana kuweza kupata
ajira. “Mimi kama Mbunge wao kama nilivyosema awali nitaendelea
kupambana na kufanya kila linalowezekana Kwa kuhakikisha Mkuranga
inakuwa sehemu ya viwanda na naendelea kitoa rai Kwa wawekezaji
kuchangamkia Ardhi yetu Kwa kujenga viwanda vingi ili vijana wangu
wapate ajira.”anasema
Anaongeza
kuwa mkuranga ilisahaulika mno pamoja kwamba ni miongoni mwa wilaya za
siku nyingi lakini imekuwa nyuma kimaendeleo hivyo niwakati mwafaka wa
kushirikiana Kwa pamoja Kwa ajili ya maendeleo. Anasema kuwa wananchi
wake waendelee kumuombea Kwa Mungu na wazidi kudumisha Umoja na
mshikamano ili Kwa pamoja wapambane Kwa lengo la kuona jimbo la mkuranga
linakuwa la mfano.
Akizungumzia
kilimo cha korosho anasema kuwa pamoja na zao hilo kuwa ndio zao
linalotegemewa kuendesha maisha ya wananchi wake lakini bado kwasababu
ya ukosefu wa kuwepo Kwa viwanda hususani vya ubanguaji kunafanya
pasiwepo na tija sana wanayoipata wananchi wake katika kilimo
hicho.Anasema kuwa kutokana na hali hiyo ana kazi kubwa ya kuendelea
kuzungumza na watu mbalimbali ili kuleta ushawishi wa kukubali Kuwekeza
kwenye ujenzi wa viwanda hivyo.
Pia
akizungumzia Elimu anasema anatambua changamoto zilizopo katika eneo
hilo hivyo amedhamiria Kwa dhati Kwa kushirikiana na Halmashauri
wanaongeza hamasa Kwa wanafunzi ili waweze kufanya vema katika masomo
yao na hatimaye kuweza kupata wataalamu wa baadae.
“Najua
kuna Changamoto ya madawati na hili tunalishugulikia Kwa kushirikiana
na kamati mbalimbali za Shule,wazazi,pamoja na walimu ili kuona namna ya
kukabiliana na tatizo hilo na hata uchakavu wa majengo .”anasema
Ulega. Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja
kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais
Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
No comments:
Post a Comment