Friday, May 6, 2016

MAMIA WAMZIKA ANDREW NICKY SANGA (KING DREW) DODOMA

Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Enzi za Uhai wake
Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga (King Drew) ukiwa unawasili katika uwanja wa Mashujaa kwa ajili ya Ibada na Kutoa kutoa Heshima za mwisho

Ibada ikiwa inaanza Baada ya Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga kuwasili
Kwaya wakiwa wanaimba wimbo wao wakati wa kujiandaa na ibada



Familia,Ndugu wa karibu, pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali wakiwa katika ibada ya kumsindikiza Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga

Mmoja wa Marafiki wakubwa wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Victor Mponzi akiwa anasoma Historia na wasifu wa Marehemu
Mmoja wa Marafiki wakubwa wa Marehemu Andrew Nicky Sanga akiwa anatambulisha wageni

Mmoja wa wageni aliyetambulishwa na alikuja na Mwili wa Marehemu kutoka Nchini Marekani
Huyu ni Rafiki yake sana na Marehemu Andrew Nicky Sanga ambaye anatoka Marekani na alikuja pamoja na Mwili akitoa salamu zake za Rambirambi kutoka Houston

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akitoa salamu zake za rambirambi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akiwa anatoa salamu za Rambirambi na kueleza namna alivyo mfahamu Marehemu Andrew Nicky Sanga

Mh. Mbunge wa Viti maalum akitoa salam za rambirambi na kusisitiza upendo kama aliokuwa nao mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga


Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani akitoa neno la Mungu la wakati wa Ibada ya kuaga Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga.












Ndugu ,Jamaa na Marafiki wakiwa katika ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga uwanja wa Mashujaa


Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wakiwa wanaaga Mwili wa Marehemu






Wadogo wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wakiwa wanamuaga mpendwa wao




Mbele ni moja ya marafiki wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga aliyetoka Marekani akitoa heshima za mwisho.




Baba wa Mzazi mwenzake na Marehemu Andrew Nicky Sanga akitoa heshima za mwisho




Mbunge wa Mikumi Mh. Joseph Haule akitoa Heshima za mwisho




Baba wa Marehemu Andrew Nicky Sanga akitoa heshima zake za mwisho kwa mwanae mpendwa




Mzazi mwenzake na Marehemu Andrew Nicky Sanga akiwa na Mtoto wao mpendwa Zoe wakitoa heshima zao za mwisho




Watumishi wa Mungu wakiongozwa na Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani wakitoa neno la Baraka kwa Marehemu Andrew Nicky Sanga






Marafiki wakubwa wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wakitoa Heshima zao za mwisho




Msafara ukielekea Makaburini




Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga ukihifadhiwa katika nyumba yake ya Milele




Umati wa watu wakiwa Makaburini kwa ajili ya Mazishi




Mh. Joseph Mbilinyi na Mh. Joseph Haule wakiwa Pamoja na Marafiki wengine wa Marehemu Andrew Sanga wakiwa Makaburini





Mama mzazi wa Marehemu Andrew Nick Sanga akiwa anaweka Shada la Maua




Baba Mzazi wa Marehemu Andrew Nicky Sanga na Mke wake wakiwa wanaweka Shada la maua




Mtoto wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wa katikati akiwa anaweka Shada la Maua




Mzazi Mwenzake na Marehemu Andrew Nicky Sanga akiwa anaweka Shada la Maua




Victor Luvena akiendelea kusoma utaratibu wa kuweka mashaja




Wazazi wa Mzazi mwenzake na Andrew Nicky Sanga wakiweka Shada




Wadogo zake na Marehemu wakiweka Shada la Maua




Mh. Joseph Mbilinyi akiweka Shada la Maua




Marafiki wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga waliokuja na Mwili kutoka Marekani wakiweka shada la Maua






Marafiki wakubwa wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wakiweka shada lao




Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani akiweka Shada




Dkt. Sanga akitoa salamu za Shukurani kwa niaba ya Familia




Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani akisoma neno la kufunga ibada










Marafiki wa Andrew Nicky Sanga wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya Mazishi




Kaburi la Marehemu mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Baada ya Mazishi





Kama kawaida wadau wa Kutwanga Foto walikuwepo wa kutosha



Picha zote na Fredy Njeje

No comments: