Monday, May 2, 2016

Makamba awasilisha Bajeti ya wizara yake na kusisistiza umuhimu wa mazingira

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma. 
 Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt. Ashatu Kijaji.
 Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
 Mashududa walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
 wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye  utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani.
 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.

(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)

No comments: