Wednesday, May 18, 2016

JESHI LA POLISI MWANZA LATOA BARAKA ZOTE ZA USALAMA KWA TAMASHA LA JEMBEKA 2016

Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa  lengo la kumkaribisha kuwa miongoni  mwa wageni waalikwa katika tamasha kubwa la Burudani JEMBEKA FESTIVAL 2016.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi Amewahakikishia  Ulinzi na Usalama wakazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake pamoja na wageni wote  watakao hudhuria tamasha la Jembeka festival  2016 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ya tarehe 21 Mei 2016 katika kiwanja Cha CCM Kirumba kilichopo  jijini Mwanza.

Kamanda Msangi ameyasema hayo  leo ofisini kwake alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (Jembejembe) Alipomtembelea kwa   lengo la kumkaribisha kuwa miongoni  mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee   nchini Tanzania.

“Napenda kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza,wageni kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na nje ya Tanzania hili ni tamasha la kipekee hapa mkoani kwetu hivyo napenda kuwaasa wananchi wote kufurahi na kuhudhulia tamasha hilo kwa furaha  pia napenda kutoa rai kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa amani”,Alisema Kamanda Msangi.

Kwa upande wake Dr. Sebastian Ndege amemshukuru Kamanda Msangi kwa ushirikiano aliouonesha tangu awali na hili la sasa kuhakikisha anaimarisha ulinzi na usalama siku hiyo ya tamasha na kuahidi kutumia vyombo vyake vya habari katika kulisaidia jeshi hilo kutoa elimu ya ulinzi shirikishi.
“Nashukuru sana kwa ushirikiano tunaoupata kutoka kwa Jeshi la polisi ngazi zote kwani wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Mwanza inakuwa salama hivyo mimi pamoja na timu yangu tunaahidi kusimama bega kwa bega na jeshi letu kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake stahiki linapokuja suala la ulinzi, usalama wa mtu mmoja mmoja na hata utoaji wa elimu kwa umma kuhusu namna ya kuzuia uhalifu, ili Mwanza yetu iwe mahali salama"
Aidha Kamanda Msangi ameahidi kuimarisha Ulinzi  wa ndani na nje  kwa maeneo yote ya wilaya ya Ilemela ambako uwanja wa CCM Kirumba ndiko unakopatikana na amewatoa hofu Wananchi wote pamoja na wageni watakaohudhuria tamasha hilo kwa kuhofia usalama. "Atakaye kuja kwa hila tutamdhibiti"
Tamasha la Jembeka festival 2016 mwaka huu litatumbuizwa na msanii kutoka nchi ya Marekani  Neyo anayetarajiwa kutua nchini kesho usiku.

Wakali wengine kutoka hapa nchini Tanzania akiwemo Diamond, Juma Nature, Ney wa Mitego, Maua Sama, Ruby, Fid q, Mo Music, Baraka da prince, na wengine kibao,  wanatarajiwa kumwaga mvua ya burudani siku hiyo.
JEMBEKA FESTIVAL linaloandaliwa na Jembe ni Jembe Entertainment kupitia Jembe FM, hufanyika kila Mwaka  mkoani Mwanza na  tamasha hilo kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu sabini toka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Katibu wa Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa  lengo la kumkaribisha kuwa miongoni  mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee  nchini Tanzania.
Aksante sana Gazeti la Mwananchi toka Mwananchi Communication kwa kutusaidia kufikisha taarifa mlango kwa mlango PAMOJA SANA.
Jumamosi hii, May 21,2016 itakuwa ni Jembeka Festival Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja na Mkali Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Pia watakuwepo wasanii wengine kibao. 
Kumbuka ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 so huu ni muda wa kununua tiketi mwana wa kwetu.
Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Mwananchi Communications,Samsung, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Binagi Blog, Michuzi Blog, DjChokaMusic.com, Lakairo Hotel na wadau wengine.

No comments: