Na Rabi Hume, Modewjiblog.
Katika
kusaidia kukamilika kwa Mpango wa Maendeleo Endelevu ambao unataraji
kumalizika 2030, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) imefanya
warsha ambayo imekutanisha wadau mbalimbali ili kuona ni jinsi gani
wanaweza kubadilishana mawazo ili kufanikisha mpango huo nchini.
Mgeni
rasmi katika warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na
Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha ambaye wakati
akifungua warsha hiyo alisema kuwa mpango huo ni muhiu wa nchi yetu kwa
sababu unakwenda kubadili maisha ya kila Mtanzania ili kuondokana na
umaskini na kuwa katika maisha bora kama jinsi malengo 17 ya mpango huo
yanavyojieleza.
Mo
Dewji Blog ilipata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo na kukuandalia
habaroi picha jinsi warsha hivyo ilivyofanyika katika ukumbi wa ESRF.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa neno la ufunguzi katika warsa iliyoandaliwa na ESRF ili
kuzungumzia Mpango wa Mendeleo Endelevu (SDG). (Picha zote na Rabi Hume,
Modewjiblog)
Baadhi
ya washiriki waliohudhuria warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii, Dkt.
Tausi Kida wakati akifungua warsha hiyo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo
akitoa neno kwa niaba ya UNDP ambao ndiyo wasimamizi wa mpango huo.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii
(ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua
Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha
Mgeni
rasmi katika warsha hiyo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua
Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha akifungua warsha hiyo
iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF).
Washiriki wakiendelea kufatilia kinachoendelea katika warsha hiyo.
Stephen Chacha kutoka Shirika la Beyond 2015 for Africa akizungumza jinsi Mpango wa SDG unaweza kufanyika nchini.
Mmoja wa washiriki, Dkt. Kitila Mkumbo akichangia mada zilizokuwa zikijadiliwa.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment