Wanafunzi Nchini hususani wale wa wa kike wameshahuriwa kujikita zaidia katika kupenda masomo ya Sayansi kwa bidii zote ili kuifanya Tanzania kufikia kwa haraka malengo yake ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Hii ni pamoja na Ukuaji wa viwanda vya ndani ambavyo vingi vitategemea ujuzi wa Sayansi na teknolojia.
Rai hiyo ametolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa mgeni rasmi wa Mahafali ya 19 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekodari ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Shule hiyo ambayo ni ya Wasichana watupu, jumla ya wanafunzi 136 wanaomaliza kidato cha sita walitunukiwa vyeti vyao vya kumaliza shule.
Dk. Kigwangalla amewapongeza wanafunzi hao 136 ambapo kati yao wanafunzi 80, ni wa mchepuo wa Sayansi ambapo amewataka kuto kata tamaa na baadala yake waongeze juhudi hadi elimu ya juu Zaidi ya ngazi ya Chuo huku pia akiwataka wanafunzi wengine hapa nchini kujikita katika masomo hayo ya Sayansi katika zama za sasa ambayo Tanzania inaelekea katika mapinduzi ya viwanda na uchumi wa Kati.
“Nina Imani na nyie. Najua hamta niangusha na mutafaulu vizuri. Nawapongeza wanafunzi wote wanaohitimu leo hii. Ni imani yangu kuwa nyote mtafaulu vizuri sana katika mitihani yenu ya kidato cha Sita kwa kupata daraja la kwanza (Division I) na wachache sana daraja la pili (Division II). Sina mashaka, najua mtailetea shule yenu (Mazinde Juu) heshima kubwa ndani na nje ya nchi” alibainisha Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa hutuba maalum ya maafali hayo.
Dk. Kigwangalla aliongeza kuwa, katika hali ya sasa ya soko la ajira kuwa gumu, aliwataka wanafunzi hao kuzingatia kipindi hiki kifupi cha kuwa nyumbani na baadae kusubiria masomo ya elimu ya juu ya ngazi ya Chuo, kuwa watakutana na vizingiti mbalimbali hivyo amewataka kuzingatia uadilifu walioupata shuleni hapo.
“Ndugu zangu wahitimu, ni kweli kwamba nchi yenu ina changamoto ya ajira. Wasomi ni wengi lakini kazi hakuna. Kwenu ninyi tayari mna sifa kwani mnaonekana mna tabia nzuri. Pia matumaini ya kufanya vizuri kwenye mtihani wenu wa taifa. Cha maana endeleeni kuwa waadilifu na chuoni mkasome bidii. Serikali inahangaika na kazi zitaendelea kupatikana tu.
Aidha, Dk. Kigwangalla alipongeza uongozi wa shule na bodi inayosimamia shule pamoja na wazazi kwa kuwezesha shule hiyo kuifikisha hapo ilipo ikiwemo katika mafanikio ya kielimu kwa wanafunzi wanaopitia shule tokea ilipoanzishwa kwake.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Sister Evetha Kilamba ameipongeza Serikali kwa ushirikiano wanaotoa kwa Shule mbalimbali hapa Nchini ikiwemo shule hiyo ambapo pia alimpongeza Mgeni rasmi Dk. Kigwangalla kwa kuwezesha kuongeza hamasa kwa shule hiyo ikiwemo harambee iliyoendeshwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Walimu shuleni hapo.
Naye Mbunge wa Lishoto, Mh. Shabani Omari Shekilindi alitoa wito kwa wanafunzi hao kuzingatia maadili mema nje ya shule na kujiandaa na elimu ya Chuo huku akiwataka kuzingatia suala la elimu katika maisha yao.
Wanafunzi hao wa kidato cha Sita wakimshangilia mwalimu wao Mkuu wakati wa mahafali hayo
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Ndugu Elishilia Kaaya akitoa maelezo machache namna wanavyoendesha shule hiyo pamoja na kuwahusia wanafunzi hao wanaohitimu
Burudani ikiendelea katika mahafali hayo.. ya kidato cha sita, St. Mary's Mazinde Juu
Bango la kuwaaga wanafunzi wa kidato cha sita kama linavyoonekana na kusomeka ambapo burudani iliandaliwa na wanafunzi wanaoingia kidato cha sita wa shule hiyo
Wanafunzi wa wahitimu wakitoa hutuba yao pamoja na kuaga shuleni hapo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba yake katika mahafali hayo huku akitoa msisitizo juu ya wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi kwa ukuaji wa uchumi
Dada Mkuu wa shule ya St. Mary Mazinde Juu akiwasha mshumaa kuashiria kwa kufunguliwa tafrija hiyo upande wa keki.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiendesha harambee maalum ya kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu. Wengine ni Mbunge wa Lushoto Mh. Shabani Omari Shekilindi (kushoto) na kulia ni Mama Amina Shamdasi ( mzazi Rasmi)
Dada Mkuu wa kwanza wa shule hiyo (Head Girl) akitoa nasaha zake kwa wanafunzi hao wanaohitimu
Mmoja wa wazazi akitoa shukrani zake katika tukio hilo. Mzazi huyo ni miongoni mwa waliojenga shule hiyo ambapo ilielezwa kuwa alichangia matofali na shughuli zingine wakati wa ujenzi wa shule hiyo wakati inaanzishwa.
Mbunge wa Lushoto Mh. Shabani Omari Shekilindi akitoa shukrani zake..
Wazazi wakilishwa keki na watoto wao katika tukio hilo
Mbunge wa Lushoto Mh. Shabani Omari Shekilindi akimlisha keki binti yake ambaye amemaliza katika shule hiyo.
Wazazi wakiwalishwa keki na wanafunzi hao
No comments:
Post a Comment