Wednesday, May 18, 2016

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA WANAHISA MEI 21

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei leo tarehe 18/05/2016 amezungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kuzungumzia kuhusu mkutano mkuu wa wanahisa wa Benki ya CRDB unaotarajia kufanyika jijini Arusha tarehe 21/05/2016 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC. 

Mkutano huo wa wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa wa Benki hiyo itakayofanyika tarehe 20/05/2016 katika ukumbi huo huo ambapo pamoja na mambo mengine wanahisa wa Benki ya CRDB watapata kufahamu juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa sehemu ya wanahisa wa Benki hiyo. 

Dk. Kimei amechukua fursa hiyo kuwakaribisha wanahisa wote wa Benki ya CRDB kuweza kushiriki katika semina na mkutano mkuu na kusisitiza kuwa mkutano wa mwaka huu utakua ni wa kipekee ikizingatiwa kuwa Benki ya CRDB ipo katika maadhimisho ya miaka 20 tangu ilipoanza rasmi mnamo mwaka 1996 baada ya utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akionyesha kitabu cha taarifa ya Mwaka ya benki hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma Shirikishi, Esther Kitoka na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay. Benki hiyo inatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanahisa Mei 21. (Na Mpigapicha Wetu)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, TullyEsther Mwambapa, Mameneja wa Idara hiyo Ena Mwangama na Godwin Semunyu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha. 

No comments: