Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (Kushoto), akikabidhi
vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia),
ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la
Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, hapo jana. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa pikipiki 2 za magurudumu
matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za
usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi
iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo
jana.Akishuhudiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki
(kushoto),akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao.
Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), akikabidhi vifaa
vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (wanne kulia),
ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la
Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, waliopo Majengo jijini Dodoma hapo jana. Wanaoshuhudia (wane kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Diwani
wa kata ya Majengo Dodoma, Msinta Mayaoyao (pili kushoto) akitoa maneno
machache katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya usafi ambapo
kikundi cha Pambana kilikabidhiwa msaada wa pikipiki 2 za magurudumu
matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za
usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana.
Akisikilizwa na afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki
(kati), Meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno (kulia) na
wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (pili kulia) kilichopo
Majengo Dodoma akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa funguo ya
pikipiki aina ya Toyo na afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio
Kaniki, (tatu kushoto), kwa ajili ya shughuli zao za usafi, kupitia
mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika
katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.
- Airtel Fursa imewapatia pikipiki mbili aina ya Guta, na vifaa vya kufanyia usafi kwa kikundi cha Pambana
Dodoma, Jumapili 1 Mei 2016, Pambana
ni kikundi cha vijana 30 wajasiriamali kinachojishughulisha na
shughuli mbalimbali katika jamii kama kukusanya taka, kuzalisha na
kusambaza sabuni na kuchomelea vyuma mjini Dodoma, ambao leo wamepokea
vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka Airtel Tanzania
kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hili limepokea vifaa
mbalimbali vikiwemo pikipiki mbili aina ya Guta, sare za kufanyia kazi,
mabuti, reki ya chuma, ufagio mgumu na vifaa vingine vya usalama vya
kufanyia kazi zao.
Afisa
uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki aliwapongeza kikundi cha Pambana kwa
juhudi zao na kufanya kazi kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya
makabidhiano alisema, " Tumeamua kutoa vitendea kazi vya usafi ili
kuweza kuungana na kikundi hiki katika kufikia lengo kuu la kuhakikisha
maeneo yanayozunguka jamii yanakuwa katika hali ya usafi na hivyo
kuchangia katika mikakati ya kutunza mazingira kwa ujumla. Sambaba na
hili Airtel imeona nia na juhudi zao kikundi hiki na ndio maana leo
imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa haraka na kukuza
biashara yao".
"Kikundi
cha Pambana kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia
Airtel FURSA na wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa
washauri wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kuimarisha biashara yao "
aliongeza Kaniki."Kama kampuni ya simu inayojali jamii yake, tumeahidi
kuwawezesha vijana hapa nchini kwa kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili
waweze kufikia ndoto zao." alisema Kaniki.
Kwa
upande mwingine kundi la Pambana waliahidi kuweka ujuzi wao wote na
kutumia kwa umakini vifaa vilivyotolewa kwao na Airtel kwa matumizi
bora na yaliyo sahihi.Kiongozi wa kikundi hicho, Amasha Zuberi,
aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika mengine hapa
nchini kuuunga mkono mpango wa Airtel katika kusaidia vijana zaidi
katika Jamii.
"Hatukuamini
siku moja tutakuwa na uwezo wa kufikia malengo yetu katika biashara
hii, tunaahidi kuweka juhudi zaidi na kutumia vifaa hivi na mafunzo
tuliyopata kwa umakini zaidi kuhakikisha tunainua zaidi biashara yetu,"
alisema Amasha.
Kwa
upande wake, wakati wa hafla ya makabidhiano, Diwani wa kata ya
Majengo, Msinta Mayaoyao alitoa wito kwa vijana kutumia program hiyo ya
Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba watanzania kuwapendekeza
vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo kwa manufaa ya
jamii zao kwani Airtel FURSA ipo kwa ajili ya kubadilisha maisha ya
vijana hapa nchini.
Airtel
FURSA, inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa
elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili
kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao.Ili kijana kushiriki au kufaidika
na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 na
kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo.
Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com. ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya kuomba msaada kutoka Airtel.
No comments:
Post a Comment