Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI wa maji na umwagiliaji mhadisi Geryson Lwenge amewaondoa hofu wananchi wa mji wa Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuhusu ahadi ya Rais Dr John Magufuli ya kumaliza kero ya maji katika mji huo wa Ilula kuwa itaanza kutekelezwa mwaka huu.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr Magufuli ni serikali ya ukweli na uwazi na ni serikali ya hapa kazi Tu hivyo kila ilichoahidi kukifanya itafanya kwa wakati na kuwataka wananchi kuendelea kujenga imani zaidi.
Waziri mhandisi Lwenge aliyasema hayo jana katika Mgahawa wa Bunge mjini Dodoma , wakati akizungumza katika kikao chake na mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na wawakilishi 11 wa wananchi wa mji wa Ilula waliofika bungeni mjini Dodoma kufuatilia ahadi ya maji iliyotolewa na Rais Dr Magufuli wakati wa kampeni kwa wananchi wa mji wa Ilula .
Mwamoto akishiriki na wananchi wa mji wa Ilula kukinga maji ambayo hutoka kwa mgao.
Alisema kuwa wizara yake imekwisha ingiza katika bajeti yake ya mwaka 2016/2017 itakayosomwa mapema wiki hii na kuwa mbali ya maeneo mengine ambayo yatapatiwa ufumbuzi wa kero ya maji mji wa Ilula ni miongoni mwa maeneo hayo .
Waziri huyo alisema kuwa lengo la serikali ni kuendelea kusogeza huduma ya maji kwa wananchi wake na kutekeleza ahadi zake kupitia ilani ya uchaguzi ya chama tawala hivyo.
Hata hivyo waziri Lwenge alimpongeza mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto na mbunge Kabati kwa kuendelea kupambana bungeni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wao na hata kufuatilia baadhi ya ahadi na kuwa hatua hiyo ni nzuri na inaonyesha ni kiasi gani wabunge wao walivyokaribu na changamoto za wananchi wao.
Mbali ya waziri Lwenge kuzungumza na wananchi hao pia mbunge Mwamoto aliwakutanisha wananchi hao na waziri wa Kilimo ,mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba ambae katika kikao chake na wananchi hao alieleza mkakati wa wizara yake kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara pamoja na wizara ya vijana na ajira ili kuanzisha viwanda vidogo vya nyanya katika mji wa Ilula na kuwa kazi ya wizara yake ni kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha nyanya na kuwawezesha wakulima hao wa mafano mpango ambao utafanyika katika kanda mbali mbali ila kwa nyanda za juu kusini wanakusudia kuufanya wilaya ya Kilolo .
Kijana wa Ilula akichambua nyanya. |
Kwa upande wake waziri wa vijana na ajira Antony Mavunde alisema kuwa wizara yake ipo tayari kuwasaidia vijana katika wilaya ya Kilolo kwani tayari wameonyesha nia ya kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo cha nyanya na kuwa kazi ambayo mbunge na viongozi wa wilaya ya Kilolo wanapaswa kuifanya ni kuwaunganisha vijana hao katika vikundi na kuanzisha Saccos zao ili pesa itakapotolewa na serikali kupitia katika saccos hiyo .
Alisema kuwa upo uwezekano wa vijana hao kuanzisha kilimo cha nyanya na kuwa na viwanda vidogo vya kuchakata nyanya na kuziuza badala ya sasa kuuza kwa hasara.
Mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto aliwapongeza mawaziri hao kwa kuonyesha utayari wao katika kuwasaidia wananchi wa Kilolo na kuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa mji wa Ilula ni maji ,masoko ya uhakika ya mazao na hivyo kusaidiwa maji na vijana kupata viwanda vidogo vidogo wataweza kukuza kilimo cha kisasa zaidi.
Katika ziara yao hiyo bungeni wananchi hao ambao ni wawakilishi wa wananchi wa Ilula waliongozana na katibu wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya ya Kilolo Bw Clemence Mponzi na aliyekuwa diwani wa Ilula Anna Msolla, Peter Mdanginyali , diwani wa kata ya Mlafu Bw Isdori Kihenge , Vicent Gaifalo,Anna Msolla, kada wa hadema Bw Khalid Muhel , Jocob Ngusulu ,Uzebeo Mhando na katibu tarafa ya Mazombe Bw King’ung’e
No comments:
Post a Comment