Muonekano wa barabara ya Nyakahura-Rusumo inayounganisha Tanzania
na Rwanda kupitia Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Mtaalam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wa pili kulia akitoa
maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa (wa tatu kulia), alipotembelea ofisi hizo katika Kituo cha pamoja
cha forodha (One Stop Border Post) upande wa Tanzania kilichopo
Rusumo wilayani Ngara, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa
ufafanuzi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (mwenye kofia) wakati akikagua
maandalizi ya ufunguzi wa Daraja la Rusumo na Vituo vya pamoja vya
forodha (One Stop Border Post) wilayani Ngara.
Muonekano wa Daraja la Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda,
kushoto ni daraja la zamani lenye rangi ya njano na kulia ni daraja jipya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
(katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya
Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale wakati akikagua
Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Meneja wa Kituo cha pamoja cha forodha(One Stop Border Post), katika
mpaka wa Tanzania na Rwanda upande wa Rwanda Bw. Moses Kalisa
akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho.
No comments:
Post a Comment