Na Woinde Shizza,Karatu
Wananchi wa kata ya mbulumbulu walalamikia Mmalaka ya hifadhi ya
Ngorongoro kushidwa kuzibiti wanyama pori kwani wanaharibu mazao yao.
Hayo waliyasema juzi wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoa
Arusha, Lekule Laizer wakati alipotembelea katika kijiji cah losteti
ikiwa ni ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho.
Walisema kuwa mazao yao yamekuwa yakiaribiwa na wanyama wanaotoka
katika hifadhi ya ngorongoro haswa nyakati za jioni na usiku na
wametoa taarifa katika uongozi wa mamlaka hiyo lakini hamna hatua
zozote ambazo wamezichukuwa.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Aron Saiteu alisema
kuwa wanyama hao wamekuwa wanakuja katika mashamba yao ambayo
wameotesha mahindi na maharage na kuingia na kula hali ambayo
inawarudisha nyuma kimaendeleo na inawakosesha chakula.
Alisema kuwa wamepeleka taarifa za malalamiko katika kituo kidogo
ambacho kipo katika eneo hilo lakini hadi sasa hamna kiongozi ambaye
amechukuwa hatua .
“awali tulikuwa tunawafukuza wanyama hawa lakini mamlaka ikaja na
kutunyima kufukuza wanyama lakini cha kushangaza mara baada ya
kutuzuia kufukuza wakatuambia tukiona mnyama tumpige simu tatizo
lililokuja ukipiga simu unaambiwa na viongozi ambao wapo apa katika
kituo cha wanyama pori cha losteti wanasema awana magari hivyo awawezi
kuja kufukuza wanyama sasa na sisi wananchi tunashindwa tufanyaje
unakuta tembo kaja au mbogo ivi unamfukuzaje jamani inabidi uache ale
akitosheka aondoke “alisema Seuri lazier
Alisema kuwa hali iyo inatokea sana hawa katika kipindi hichi mazao
yao yametoka na wananyama hao usogea maeneo hayo kuanzia majira ya saa
kumi na mbili jioni na hata saa kumi na mbili asubui unaweza ukawakuta
wananyama hao wakiwa mashambani kwa watu.
Aidha aliongeza kuwa kunakituo cha ngongoro kipo karibu na kijiji
hicho na pindi wanapopiga simu pale ili wapatiwe ufumbuzi wa
kufukuziwa wanyama hawa wamekuwa wakijibiwa kuwa ofisi hiyo haina gari
na badala yake wanawaambia wananchi wapige simu makao makuu ya
hifadhi kuomba gari litakalo saidia doria ya ulinzi wa mashamba juu
ya wanayama pori .
Aidha walifafanua kuwa kwakuwa tatizo hili limekuwa linatokea mara
kwamara wanaomba basi serekali au mamlaka husiku kusaidia kulipa
angalau fidia ya nusu ya mazao ambayo yameliwa na wanyama hawa ili
angalau mwananchi asipate hasara ya moja kwa moja .
Akiongelea swala hilo mkuu wa idara ya uhifadhi ambaye pia ni kaimu
muhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo Izrael Namani alisema kuwa swala hilo
sio la kweli kwani kwanza kabisa mamlaka ina ofisi pembezoni mwa
kijiji hicho kinacholalamikiwa huku akisema kuwa pia mamlaka ina gari
ya kufanya doria za mara kwa mara katika mipaka yote ya hifadhi .
Alisema kuwa pia swal ahili lipo chini ya idara ya wanyama pori lakini
wao kama hifadhi ya ngorongoro kupitia idara ya ujirani mwema wamekuwa
wakishirikiana kw aukaribu na wananchi katika kufanikisha mambo mengi
ikiwemo ya wanyama kutoharibu mazao.
Aliongeza kuwa pamoja kuna changamoto mbalimbali lakini pia
wanajitaidi kwa hali namali kuhakikisha wanayama wanakaa katika maeneo
yao na kutoleta mathara kwa wananchi na mali zao.
“unajua kwa mipaka ya hifadhi ni mingi na sio mda wote unaweza kuta
askari yupo katika kila eneo lakini pindi tunapopata taarifa tunatuma
askari wetu wawanyama pori na waenda kwa muda unaotakiw akutatua
tatizo hilo mfano ata awa wananchi wakipiga simu kiukweli apa nata
nizungumzie swal ala gari ndugu mwandishi umeona geografia ya hayo
maeneo kuna sehemu ambayo gari aiwezi fika sasa apo kweli unafanya
inabidi ufike gari inapofika alafu uanze kutembea na miguu lakini
swala ambalo wanasema atuwapi ushirikiano sio kweli’alisema Namani.
Aidha alisema kuwa kwa upande wa swal ala fidia wao kama mamlaka ya
ngorongoro hawana fidia yeyote wanao toa ila kuna mkono wa pole ambao
unatolewa kwa muadhirika kutoka kwa mamlaka ya idara ya wanyama pori
na hiii sio fedha iliopangwa ni kiasi Fulani bali ni chochote kile
kitakachopatikana.
Gazeti hili lilimtafuta pia Afisa maliasili wa wilaya ya katatu Staley
Mruma ambaye yeye pia ni mlengwa mkuu anaesimamia wanyama pindi pale
wanapotoka nje ya hifadhi naye alisema kuwa wao kama idara ya
maliasili kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro wamekaa
kikao march 19 cha kuangalia jinsi ya kukabiliana na tatizo hili na
walikubaliana kushirikiana kutatua tatizo hili na kufuta kauli ya
kusema wanyama ni wa mamalaka fulani bali waliamua kwa pamoja kwa
kusema wanyama ni wawatu wote.
Alibainisha kuwa kwa sasa ivi wameweka mikakati wa kufanya doria kwa
pamoja wao pamoja na hifadhi ya ngorongoro ,pia waliagiza magari
yaongezwe ili yafikie nane ambayo yataweza kufikia katika kila mpaka
,huku akibanisha kuwa katika kikao hicho pia walipanga kufanya vikao
vinne kila mwaka kwa ajili ya kujadili changamoto zilizopo katika
mipaka ya hifadhi hiyo.
Aidha alisema kuwa kwa upande wa malipo au fidia ambazo wanalalamikia
wananchi wao kama idara ya maliasili wanamfuko wa kutoa pole na
mpaka sasa unafanya kazi kwani kipindi cha mwaka jana mwezi wasita
waliwalipa kifuta jasho wananchi ambao wamearibiwa mazao yao ambapo
alisema jumla ya wananchi 52 walilipwa kifuta jasho hicho.
"kuna wananchi ambao tumeshawalipa kifutajasho kutokana na kuaribiwa
mazao yao na wanyama lakini sio wote kunabaadhi ambao bado awajalipa
walishaleta malalamiko yao na sisi tukayapeleka wizarani kwa iyo
tunasubiri majibu yakija tu hivi tutawalipa kifutajasho chao"alisema
mruma.
Aidha aliongeza kuwa katika watu hao wanaodai kifutajasho chao kuna
wananchi sita ambao hawajalipwa kwani wao walifariki mara baada ya
kuzuriwa na wananyama tofauti tofauti kwa nayakati tofauti lakini sio
kwamba hawata lipwa na swala lao lilishapelekwa wizarani na wanasubiri
kifuta jasho chao kije na kikifika watalipwa ndugu zao.
Alibaini vijiji ambavyo vilikuwa vinadai fidia na baadhi yao
vimeshalipwa kuwa ni pamoja na kambi ya simba ,kitete,lostate pamoja
na slahamu huku akisema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kwani wao
kama maliasili kwa kushirikiana na hifadhi ya ngorongoro wanaakikisha
kunakuwa na ulinzi wa kutosha.
No comments:
Post a Comment