Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom
Nyanduga (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki
wa warsha ya wadau wa masuala ya haki jinai (criminal justice) kutoka
idara mbalimbali za Serikali na Asasi Zisizo za Kiserikali, muda mfupi
baada ya kufungua warsha hiyo, iliyofanyika Makao makuu ya ofisi za
Tume, jijini Dar es Salaam mapema leo (Aprili 11, 2016).
Warsha hiyo ya siku moja iliandaliwa na THBUB kwa ushirikiano na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) na Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI) ya nchini India. Ililenga pamoja na mambo mengine kuwahamasisha wadau kujiunga na kushiriki katika jukwaa la Haki na Usalama (justice and security forum) linalotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mfumo wa haki jinai nchini.

Mkurugenzi wa Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI) ya
nchini India, Bibi Maja Daruwala akiongea wakati wa warsha ya wadau wa
haki jinai, Makao Makuu ya Ofisi za THBUB, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika warsha hiyo.
Picha ya pamoja
Mhe. Nyanduga na wageni wake, Bibi Daruwala, Mkurugenzi wa Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative na Bwana Anthony Adam, afisa kutoka Asasi ya Open Society Institute of Eastern Africa wakifurahia jambo muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa haki jinai iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Germanus Joseph wa THBUB)
Mwenyekiti
wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akibadilishana mawazo na wabia wa
mradi (project partners). Kulia kwa Mhe. Nyanduga ni Mtendaji Mkuu wa
Chama cha Wanasheria Tanzania Bara, Bwana Kaleb Lameck Gamaya na kushoto
kwake ni Mkurugenzi wa Asasi ya Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI), Bibi Maja Daruwala. Kulia ni Bwana Ula Dzenisevich, afisa kutoka CHRI.
Mratibu
wa Mradi, Bwana Stephen Msechu akitoa maelezo kuhusu jukwaa la Haki na
Usalama wakati wa warsha ya wadau wa haki jinai iliyofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa
warsha ya haki jinai mapema leo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wajumbe akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment