Na John Nditi, Morogoro
MWENGE wa Uhuru umemaliza mbio zake mkoani Morogoro na umekabidhiwa mkoa wa Tanga mnamo Apriili 25 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na mbio zake katika muda wa siku kumi kwenye Halmashauri 11 zilizomo mkoani humo, imeelezwa.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kabwe aliukabidhi Mwenge wa Uhuru na wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mkuu wa mkoa mwezake wa Tanga, Martine Shigela , katika Kijiji cha Kikunde,kilichopo wilayani Kilindi .
Kijiji cha Kikunde kilichopo katika wilaya hiyo kinapakana na kijiji cha Iyogwe kilichopo wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro.
Kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa mkoa mwezake huyo, Dk Kebwe alisema , Mwenge wa Uhuru ulipokuwa mkoani Morogoro ulipitia miradi 41 yenye thamani ya Sh bilioni 9.4 ikiwa ni ya kuonwa , kuwekewa mawe ya msingi na kuzunduliwa.
Mwenge wa Uhuru ulizinduliwa katika mkoa wa Morogoro , Aprili 18, mwaka huu na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan , katika uwanja wa Jamhuri wa mjini Morogoro na kukimbizwa kwenye halmashauri saba kati ya nane zilizopo mkoani humo.
Kauli mbiu za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu (2016): “ Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa , Washirikishwe na Kuwezeshwa “.
Naye Mkuu wa mkoa wa Tanga, Shigela,alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani humo utapitia miradi 78 yenye dhamani ya Sh bilioni 22.7 na utakimbizwa kwa muda wa siku 10 katika halmashauri 11 zilizomo mkoani humo na mara baada ya kukabidhiwa ulianza mbio zake katika wilaya ya Kilindi.
Baadhi ya wakuu wa Idara katika wilaya ya Gairo na mkoa wa Morogoro wakijadiliana jambo, huku wananchi wakishangiliwa Mwenge wa Uhuru eneo la Kituo cha Afya Gairo.
Eneo la kijiji cha Kilindi, mkoa wa Tanga , ambapo shughuli za makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kuendelea na mbio zake mkoa wa Tanga kutoka Morogoro zilifanyika Aprili 25, mwaka huu.
Furaha ya wauguzi na madaktari wa Kituo cha Afya Gairo , wakati Mwenge wa Uhuru ulipozuindua jengo la wodi ya wanaume , Aprili 24, mwaka huu ( mwenye kushika karatasi ) ni Mkuu wa wilaya ya Gairo, Khanifa Karamagi.
Kujiweka sawa.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe ( kushoto) akitoaa taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru wakati ulipokibizwa mkoani huo wakati wa kumkabidhi Mwezake wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe akipasha mwili sambamba na mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa , Aprili 25, mwaka huu kabla ya kumkabidhi Mwenge huo mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga , Martine Shigela akifurahia jambo kabla ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na viongozi wake wa kitaifa kuanza mbio zake mkoani humo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela akitoa salamu za Mwenge wa Uhuru na kuwakaribisha wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa kuanza mbio zake katika halmashauri 10 kati ya 11 za mkoa huo.
RC Morogoro akipasha mwili eneo la mpakani wa mkoa wa Morogoro , wilaya ya Gairo na mkoa wa Tanga , kijiji cha Kikunde , wilaya ya Kilindi.
RC Tanga , Martine Shigela akishika Mwenge wa Uhuru kabla ya kuukabidhi wa mkuu wa wilaya ya Kilindi.
RC Tanga , Martine Shigela akishika Mwenge wa Uhuru kabla ya kuukabidhi wa mkuu wa wilaya ya Kilindi.
RPC Tanga, Leonard Paulo ,akishika Mwenge wa Uhuru.
Timu ya mkoa wa Morogoro ikiongozwa na mkuu wa mkoa, Dk Kebwe.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wakisubiri zamu ya kukaribishwa mkoa wa Tanga kutoka Morogoro.
Wakuu wa mikoa , Morogoro pamoja na Tanga wakikabidhiana Mwenge wa Uhuru mpakani mwa mikoa hiyo , Aprili 25, mwaka huu.
/var/folders/z5/3w95s8nx4yvgnn6qf4qgw4f80000gn/T/com.apple.Preview/com.apple.Preview.PasteboardItems/Wanafunzi shule ya Msingi Kibedya, wilaya ya Gairo wakishikihswa Mwenge wa Uhuru.
No comments:
Post a Comment