Jumapili ya tarehe 24 April wanawake mbali mbali wa jiji la Dar es salaam walikutana pamoja kuadhimisha miaka mitano toka kuanzishwa kwa kitchen party gala."Kitchen party gala event imetokana na zile shughuli za kitchen party anazofanyiwa bi harusi mtarajiwa kufunzwa maisha ya ndoa.Lakini sisi tukasema kila mtu anahitaji mafunzo hayo kila inapobidi ikiwemo mahusiano,ndoa,ujanajike/uanamke,kujitambua,kujisimamia,kazi,familia,afya,ujasiriamali n.k.
Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Sheria,kilichopo karibu na kituo cha mawasiliano ,Ubungo nyuma ya jengo la Mawasiliano Tower,tamasha hilo lililokuwa limebeba ujumbe "MWANAMKE......CHUKUA HATUA acha kulala na kuzubaa.Saa mbaya hizi kamata usukani wa maisha yako,lilionekana kuwavutia sana akina dada na akina mama kutokana na namna lilivyokuwa limeandaliwa.
Mwanamke amezungukwa na mambo mengi sana ambayo kila wakati anahitaji kukumbushwa na kufundishwa ikibidi ndio tukaanza KITCHEN PARTY GALA 2011 mpaka Leo 2016 " Alisema Dina Marios moja ya waandaaji wa tukio hilo akishirikiana na Vida Mndolwa. "Tumelidesign Tamasha letu liwe la kuelimisha na kuburudisha pia ili kukufanya urelax na ufurahi na kila utakachosikia usikisahau." Aliongeza Dina Marios.
Baadhi ya Washiriki wa kitchen party gala wakifurahia jambo huku wakibadilishana mawazo.
Mmoja wa wasemaji wa Hafla hiyo Dkt.Peter Mitimingi ambaye ni mtaalamu katika nyanja mbalimbali ikiwemo mambo ya uongozi,ushauri,biblia,saikolojia na pia ameandika vitabu vingi tu vya mafunzo na ushauri.
Pastor Debora Kaisi akitoa neno katika hafla hiyo ya Sherehe za miaka 5 ya kitchen party gala.
Baadhi ya Washiriki wa kitchen party gala wakiserebuka kwa pamoja huku wakibadilishana mawazo.
Akina mama waserebuka kwa raha zao
wengine wakiserebuka huku wakibadilishana mawazo ya hapa na pale
Walipoguswa na mada yoyote hawakusita kuonesha hisia zao.
Mratibu wa Sherehe za miaka 5 ya kitchen party gala Dina Marios akitoa mwongozo mfupi wa shughuli nzima ukumbini.
Washiriki wakifuatilia jambo kwa umakini ukumbini humo.
Akina mama Wakiserebuka kwenye hafla hiyo
Coach James Mwang'amba kazi yake ni kucoach katika masuala ya ujasiriamali,kujisimamia na mbinu mbali mbali za kufanikiwa katika maisha.
Akina Mama wakiserebuka kwa raha zao
Wengine walionekana kufurahi zaidi.
Mida ya misosi iliwadia.
Brand manager wa jubilee insurance Bi Harieth Kileo
No comments:
Post a Comment