Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akitoa
ufafanuzi wa utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa
Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi
wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 31, 2016.
Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu (wa kwanza kulia) Erick Shitindi (Kazi na Ajira), Dkt. Hamis Mwinyimvua (Sera) na kushoto ni Mussa Uledi (Bunge) wakifuatilia hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) walipokutana na ofisi hiyo tarehe 31 Machi, 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akimsikiliza Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe.Najma
Giga (kushoto) wakati kamati hiyo ilipokutana na Ofisi ya Waziri Mkuu
katika Ukumbi wa Ofisi hiyo tarehe 31 Machi, 2016.
Mratibu
wa Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za
Kifedha Vijijini Bw. Walter Swai akiwasilisha utekelezaji wa programu
hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa mikutano wa
Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 31, 2016.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.jen. Mbazi Msuya
akiwasilisha masuala ya menejimenti ya maafa katika mkutano wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Ukumbi wa mikutano wa
Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 31, 2016.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Rashidi Shangazi
(mb) akichangia hoja wakati Kamati hiyo ilipokutana na Ofisi ya Waziri
Mkuu katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Machi 31, 2016.
Ofisi ya Waziri Mkuu imewasilisha Utekelezaji wa Miradi mitatu inayoiratibu kwa Kamati ya Bunge na Sheria; Miradi hiyo ni Programu
ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha
Vijijini Mradi wa Taarifa za Hali ya Hewa na Uboreshaji wa Mifumo wa
Taadhali za Awali pamoja na Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Nchi katika
kujiandaa na kukabiliana na maafa.
Akitoa
ufafanuzi wa miradi hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) kwa Kamati
hiyo ya Bunge Machi 31, 2016 ilipokutana na Ofisi ya Waziri Mkuu,
alibainisha kuwa miradi hiyo inalenga kupunguza umasikini na kujenga
uwezo wa Serikali katika Menejimenti ya Maafa
Mhagama
alifafanua kuwa Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani
na Huduma za Kifedha Vijijini Mradi niya miaka saba ambayo utekelezaji
wake ulianza mwaka 2011, lengo la programu hiyo ni kufanikisha adhima ya
serikali ya kupunguza umasikini na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi
endelevu kwa kuziwezesha kaya za vijijini kujiongeza kipato na usalama
wa chakula
"Programu
itafanikisha malengo yake kwa kuboresha miundo mbinu ya masoko,
kuongeza thamani mazao ya kilimo, kupanua wigo wa huduma za kifedha
zipatikanazo vijijini na kuwajengea wananchi waishio vijijini uwezo wa
kuyafikia masoko"alisema Mhagama
Kwa
upande wa Mradi wa Taarifa za Hali ya Hewa na Uboreshaji wa Mifumo ya
Taadhali za Awali alibainisha kuwa, mradi huo unalenga kuimarisha uwezo
wa nchi katika kukusanya takwimu za hali ya hewa na mabadiliko ya tabia
nchi yanayoweza kusababisha maafa.
"Pia
mradi utasaidoia kuboresha mifumo ya utoaji wa taarifa za awali ili
kuzuia au kuhimili athari za majanga yanayoweza kusababishwa na
mabadiliko ya tabia nchi".Alisisitiza
Aliongeza
kuwa Kuimarisha Uwezo wa Nchi katika kujiandaa na kukabiliana na maafa
unalenga kuongeza uwezo wa Serikali na Taasisi zake katika Menejimenti
ya Maafa na kuboresha ufanisi wa Mamlaka za Serikali za mitaa katika
kujiandaa na kukabiliana na maafa.
Makamu Mwenyekiti
wa Kamati hiyo mhe. Najma Giga (mb) alibainisha kuwa wameridhishwa na
utekelezaji wa miradi hiyo, na kupendekeza kuwa miradi hiyo iongeza
nguvu Vijijini katika utekelezaji wake ili iweze kuwafikia wananchi
wengi zaidi.
"Mjitahidi
kuitangaza miradi hii ili wananchi wengi waifahamu na waendelee
kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake na hatimaye taifa letu
litaweza kupunguza umasikini lakini pia kujenga uwezo wa menejimenti ya
maafa" Alisema Giga.
No comments:
Post a Comment