Tuesday, April 5, 2016

NAIBU WAZIRI WAMBURA AIAGIZA BMT KUONGEZA KASI YA KUFUATILIA VIWANJA VYA MICHEZO VILIVYOVAMIWA


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akipokelewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alipofanya Ziara katik ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura aakizungumza na wafanyakazi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alipofanya Ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Bibi. Nuru Halfani Mrisho Milao akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Annastazia James Wambura (katika) katika ofisi za Baraza la Taifa la Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja.
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Utumishi wa BMT Bw. Jacob Nduye na wapili kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura, Naibu Katibu Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja wakati wa ziara yake katika ofisi za Baraza hilo lep jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa BMT leo jijini Dar.Kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo na wa mwisho kulia waliokaa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja.Picha na: Frank Shija, WHUSM


Na: Frank Shija, WHUSM

BMT yaagizwa kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa viwanja vya michezo vilivyovamiwa nakuvirejesha kwa jamii kwa ajili ya matumizi ya michezo.

Agizo hilo limetolewa leo na na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nuru Khalifani Milao alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo kwa ajili ya kujionea hali ya utendaji katika baraza hilo.

Mhe. Wambura alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya maeneo mengi yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii ikiwemo michezo kuvamiwa na watu na kufanya shughuli kinyume na taratibu.

“Kama ilivyo katika Ilani ya uchaguzi BMT mnawajibika kufuatilia maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za michezo fuatilieni kwa karibu kikiwemo na kile cha Tandika ambacho tulikwisha anza nacho” Alisema Naibu Waziri.

Aidha Wambura alihimiza Bmt kuhakikisha inahamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo kwa kuwa michezo ipo kwa ajili ya wote na kuongeza kuwa mbali na mashindano michezo pia utumika kujenga afya za mwanadamu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo watahakikisha wanapiga hatua katika kukuza sekta ya michezo kwani BMT ndiyo mkono pekee wenye dhamana ya kusimamia michezo kisheria.

Ata hivyo alielezea changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao kuwa ni kuwa ni ufinyu wa bajeti, upungufu wa wafanyakazi na muingiliano wa Wizara mbili katika utekelezaji katika ngazi ya Manispaa na Halmashauri Maafisa Michezo wanawajibika chini ya Wizara ya TAMISEMI hivyo kuna haja ya kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya kushirikiana.

No comments: