Sunday, April 17, 2016

MBUNGE HASNA MWILIMA ATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 6 NA TANI 17 ZA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO KIGOMA

Na Editha Karlo wa blog ya Jamii, Kigoma

MBUNGE wa Jimbo la kigoma Kusini ,Hasna Mwilima amewakabidhi msaada wa shilingi milioni sita na laki tatu na tani kumi na saba za vyakula kwa wahanga wa mafuriko katika Kijiji cha Kirando kata ya Sunuka Wilayani Uvinza.

Akizungumza na Wananchi wa kijiji hicho wakati akikabidhi misaada hiyo iliyo tolewa na Halmashauri ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma na wadau mbalimbali alisema serikali kwa kuwathamini wananchi imeamua kutoa misaada ilikuweza kuwasaidia wahanga waliopoteza mali zao wakati wa mafuliko.

Mwilima alisema anaupongeza uongozi wa Mkoa wa kigoma na halmashauri zote kwa kutoa msaada wa vyakula vitakazo wasaidia waathirika hao katika kipindi hika ambacho wanajipanga kurekebisha makazi yao.

Pia aliishukuru Halmashauri ya Uvinza kwa kuthamini Wananchi wake na kutoa msaada wa shilingi milioni tano na Mwenyekiti wa Halmashauli hiyo kuongezea laki mbili wameonesha jinsigani serikali ya awamu ya tano inavyo wathamini wananchi.

“mimi kama mbunge wenu nitatoa shilingi milioni moja nitaongezea katika mchango wa Viongozi wengine waliotoa tutahakikisha tunashirikiana katika wakati waraha, wakati washida na nyakati zote tupo pamoja nitawahudumia ipasavyo ndugu zangu “, alisema Hasna.

Hata hivyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuchangia Chakula tani saba kupitia michango iliyotolewa na Halmashauri zote za Mkoa ilikuweza kuwasaidia Wanakijiji waliokumbwa na mafuriko.

Rehema Hassani ni mmoja kati ya Wahanga wa mafuriko pia ni Mkazi wa Kirando alisema kwaniaba yawanakijiji wenzake wanaishukuru Serikali pamoja na Mbunge kwa kutoa misaada hiyo tunaimani itatusaidia na tutaweza kujipanga upya na kuziendesha familia zetu.

Aliiomba Serikali kuwapatia maeneo mengine waweze kujenga na kuondoka kuishi mabondeni ambapo mvua kubwa ikinyesha maji hujaa mtoni na kuingia ndani kupelekea mafuriko hivyo serikali igawe maeneo mengine yakuweka makazi.

Msaada uliotolewa ni maharage kilo218,mchere kilo1240, unga , mihogo,mahindi, mashuka kwaajili ya zahanati 218,na mafuta ya kupikia na chumvi na shilingi milioni sita na laki tatu watakazo gawiwa wahanga wa mafuriko hayo zilizo tolewa na serikali pamoja na wadau mbalimbali.

Mafuriko hayo yalitokea tarehe 13 mwezi wa pili mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyonyesha uharibifu mkubwa wa mali na kaya zipatazo 49 kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji.
Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini Husna Mwilima akimkabidhi fedha shilingi. Milioni sita na laki tatu mwenyekiti wa kijiji cha Kirando Athumani Chuma kwaajili ya wahanga wa mafuriko katika kijiji hicho.
Mhe. Hasna Mwilima akimkabidhi Bi rehema Issa mfuko wa sembe mmoja wa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha kirando.
Mhe. Hasna akiteta jambo na muathirika wa mafuriko katika kijiji cha Kirando.
Sehemu ya chakula tani kumi na saba zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la kigoma kusini Hasna Mwilima kwa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Kirando.
Baadhi ya makazi ya wanakijiji cha Kirando yaliyokumbwa na mafuriko

No comments: