Tuesday, April 5, 2016

MAFURIKO YAZIKOSESHA MAKAZI KAYA 100 ENEO LA CHALINZE NYAMA DODOMA, YAFUNGA BARABARA

Baadhi ya Nyumba za makazi, huduma mbalimbali na vijiwe vya kufanyia biashara eneo la Chalinze nyama Dodoma vikiwa vimezingirwa na maji (mafuriko) kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo usiku wa kuamkia April 4, 2016.
Baadhi ya Wakazi wa eneo la Chalinze nyama Dodoma wakihamisha mali zao baada ya makazi yao kuzingirwa na maji (mafuriko) kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo usiku wa kuamkia April 4, 2016.
Baadhi ya magari ya kubeba abiria mapema leo yalinusurika kusombwa na mafuriko yalipojaribu kuvuka barabara eneo la Chalinze nyama Dodoma kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia April 4, 2016.
Safari za magari ya abiria na mizigo zilikwama eneo la Chalinze nyama Dodoma kwenye barabara itokayo Dodoma kuelekea Dar es salaam kuanzia alfajiri ya Aprili 4, 2016 hadi alasiri kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Farida Mgomi (katikati) na viongozi wengine wakikagua eneo la Barabara eneo la Chalinze nyama ili kuona namna ya kupitisha magari ya abiria na mizigo yaliyokwama tangu alfajiri ya Aprili 4, 2016 hadi alasiri kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo.
Magari ya abiria na mizigo yanayokadiriwa kuwa zaidi ya 1,000 ambayo yalikwama eneo la Chalinze nyama Dodoma kwenye barabara itokayo Dodoma kuelekea Dar es salaam kuanzia leo alfajiri hadi alasiri kufuatia barabara hiyo kufungwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo April 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akishuhudia magari ya mizigo na abiria yakiendelea na safari Leo Alasiri baada ya kuruhusiwa kufuatia kupungua kwa maji (mafuriko) yaliyofunga barabara kuu ya Dodoma Dar es salaam eneo la Chalinze nyama Dodoma tangu alfajiri.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (kushoto) akiijulia hali kaya iliyonusurika kusombwa na mafuriko kufuatia makazi yao kuzungukwa na maji mengi eneo la chalinze nyama yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo April 4, 2016.

No comments: