Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akipima BP kwa madereva wa masafa wakati wa uzinduzi wa kituo cha Wenda |
Mwakilishi wa Impala Jorge Rico Grillo akizungumza na wanahabari |
Mwakilishi wa makampuni ya usafirishaji Bw Arif Abri akieleza faida ya vituo hivyo kwa madereva |
mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Masenza akijiandaa kukata utepe |
Uzinduzi wa kituo cha Ilula |
Add caption |
Mkuu wa mkoa wa Iringa akipima BP |
Na MatukuiodaimaBlog
MADEREVA
wa malori nchini wametakiwa kutumia vituo vya upimaji virusi
vya UKIMWI (VVU) kwa hiari kupima afya zao katika vituo
vilivyojengwa kandokando ya barabara kuu ya kuanzia Jijijini Dar es
Salaam hadi Tunduma mkoani Mbeya.
Ria
hiyo imetolewa juzi na mwakilishi
wa makampuni ya usafirishaji mizigo Bw Arif Abri kutoka kampuni ya
FM Transporter wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Ilula wilaya ya
Kilolo na Wenda kilichopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa ,kuwa
matumizi sahihi ya vituo hivyo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa
madereva na familia zao.
Kwani
alisema kuwa hakuna udereva salama kama madereva hawatakuwa na tabia
ya kujua
hali za afya zao kupitia vituo hivyo ambavyo pia madereava hao
watavitumia kupima na kutibiwa bure magonjwa mbali mbali.
Alisema
madereva hao wakijua afya zao
itawawezesha kufanya maamuzi ya busara yanayoweza kusaidia mikakati
mbalimbali ya serikali ya kupunguza hasara na vifo vinavyotokana vya
ajali zinazotokana na madereva hao kutokuwa na afya njema.
Hata
hivyo alisema pamoja na vituo hivyo kuwalenga madereva bado
wananchi wanaozunguka vituo hivyo wataweza kupata huduma hiyo
bure na kuwa huduma katika vituo hivyo itatolewa kwa haraka zaidi.
Huku meneja wa
kampuni ya Impala Terminals Tanzania ambayo ni sehemu ya wadau hao,
Jorge Rico Grillo alisema kampuni yao kwa kushirikiana na mashirika ya
Puma Energy Foundation na Trafigura walitoa fedha kwa shirika la
kimataifa linalojishughulisha na afya la North Star Alliance na kujenga
vituo hivyo.
Alisema pamoja na vituo hivyo viwili, wadau
hao wamejenga vituo vingine vinne katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya
vilivyozinduliwa kwa nyakati tofauti wiki iliyopita.
Alisema
lengo lao ni kuona madereva wanaotumia barabara hiyo inayokwenda hadi
nchi za Malawi na Zambia wanakuwa katika mazingira rafiki
yatakayowawezesha kupata ushauri na huduma mbalimbali za afya wakiwa
safarini.
Mwakilishi wa shirika la North Star Alliance, John
Mwachama alisema kwa kupitia vituo hivyo madereva watapata elimu ya
afya, madhara ya dawa za kulevya na pombe pamoja na huduma bure ya
upimaji na matibabu wa magonjwa mbalimbali ikiwemo VVU, kisukari na
mengineyo jambo litakalowawezesha kuchukua tahadhari kabla na wakati
wakitumia barabara hiyo.
Meneja Uendeshaji wa Puma Energy
Tanzania, Lameck Hiliyai alisema kujengwa kwa vituo hivyo kutasaidia
makampuni ya usafirishaji kuwatumia madereva wanaojali afya zao.
Akizindua vituo hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema
vituo hivyo vitakuwa vya manufaa sana kwa madereva na wananchi walio
jirani navyo kwani vinaongeza upatikanaji wa huduma zinazotolewa pia
katika vituo vingine binafsi na vya serikali.Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akizindua vituo
hivyo alipongeza wadau hao kwa kujitolea kujenga vituo hivyo na
kutaka watendaji wa vituo hivyo kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa
badala ya kuanza kuiba madawa.
Vituo
hivyo ambavyo pia vitatoa huduma kwa wananchi wanaovizunguka,
vimejengwa katika mji mdogo wa Ilula, wilayani Kilolo na kijiji cha
Wenda, Iringa Vijijini kwa msaada wa wadau wa sekta ya usafirishaji
nchini watakaogharamia uendeshaji wake hadi mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment