Monday, April 25, 2016

LUBUVA AKABIDHI MIKANDA,VIRUNGU VYA ULINZI NA MAKOTI YA MVUA KWA WANAKIKUNDI CHA ULINZI SHIRIKISHI OYSTERBAY JIJINI DAR.

 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva awakabidhi mikanda, virungu na makoti ya kujikinga na mvua kwa wanakikundi cha ulinzi shirikishi cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Pia alizungumza na wananchi wa mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam ili kujua changamoto za wananchi wa mtaa huo katika nyaza za ulinzi, usalama na Usafi wa mazingira.

 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akifafanua jambo alipokuwa akisoma ripoti ya Mtaa wake katika ulinzi , usalama na usafi wa mazingira ya mtaa wa Oyster bay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Oysterbay, Achema Kalembo akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya Mtaa wa Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva alipokuwa akizungumza na wanamtaa huo ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.
Baadhi ya wananchi wakichangia maada katika mkutano wa  wananchi wa  Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akiwakabidhi Virungu, Mikanda na Makoti kwa wanakikundi cha ulinzi shirikishi wa mtaa wa Osyterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  
 Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Oysterbay, Achema Kalembo  akizungumza na mwandishi wetu mara katika mkutano wa wananchi wa mtaa wa Oysterbay  walipokuwa wakizungumza na   Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Meza kuu wakisikiliza hoja za wananchi. 
 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya kukabidhi mikanda, virungu na makoti kwaajili ya mvua kwa wanakikundi cha Ulinzi shirikishi wa mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments: