Matukio haya na yale sambamba na habari/picha za ziada za Globu ya Jamii
Wednesday, April 13, 2016
LANCET TANZANIA LIMITED YAWAPIGA MSASA MADAKTARI NA WAUGUZI HOSPITARI YA RUFAA YA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI
Mtafiti
wa Magonjwa mbalimbali Dkt Ahmed Kalebi akizungumza na madaktari na
wauguzi wa Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi wakati
wa warsha juu ya matumizi ya maabara ya kisasa iliyofunguliwa mjini
Moshi kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali.
Baadhi
ya Madaktari na wauguzi katika Hospitari ya Rufaa ya mkoa wa
Kilimanjaro ya Mawenzi wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Dkt
Ahemd Kalebi wakati wa warsha hiyo iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa
ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.Dkt
Kalebi akisisitiza jambo wakati akizungumzia juu ya ufanyaji wa vipimo
kwa magonjwa kama saratani na magonjwa mengine ambayo wagonjwa wengi
wamekuwa na tabia ya kwenda kutafuta matibabu nje ya nchi.
Baadhi ya Madaktari na Wauguzi katika Hospitari ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi wakiwa katika Warsha hiyo. Kaimu
Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Josephat Bniface akizungumza
jambo katika warsha hiyo ya siku moja iliyoenda sanjari na ufunguzi wa
maabara ya kisasa ya Lancet iliyofunguliwa mjini Moshi. Mtafiti
wa magonjwa mbalimbali ,Dkt Ahmed Kalebi akizungumza na wanahabari
kuhusiana na mada aliyowasilisha katika warsha hiyo.Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment