Tuesday, April 5, 2016

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA)

 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria walipowasili katika ofisi za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika ziara ya kujionea shughuli za Mamlaka hiyo.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisalimiana huku wakielekea  katika ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),jijini  Dar es salaam kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo. 
 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji Bi. Sarah Kibonde Msika akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria walipofika kutembelea ofisi za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), jijini Dar es salaam, hivi karibuni.
 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mhe. Antony Mavunde akieleza jambo wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ziara ya Kamati ya bunge ilipotembelea ofisi za SSRA, Kamati  inayoongozwa na Mh. Mohamed Omary Mchengerwa (pili kulia). 
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge Kudumu wakitemebelea vitengo mbalimbali   ndani ya ofisi za SSRA. 
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akitoa mada na maelezo mbalimbali kuhusu Mamlaka pamoja na Sekta nzima kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria ilipotembelea ofisi za SSRA, Dar es salaam hivi karibuni. 
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Katiba na Sheria wakiwa na uongoziwa SSRA pamoja na  viongozi  toka Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu ), wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za SSRA. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akihojiwa na waandishi toka vyombo mbalimbali vya habari baada ya kikao kilichofanyika wakati kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria ilipotembelea Mamlaka hiyo. 
 Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria ikiongozwa na Mh.Mohamed Omary Mchengerwa aliyekaa (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mhe. Antony Mavunde. Kati ya waliosimama Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA Bw. Juma Muhimbi (wan ne kulia) akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka (kushoto) pamoja na menejimenti ya SSRA.

No comments: