Thursday, April 7, 2016

JUMA NATURE AJIPIGA PINGU JEMBEKA FESTIVAL 2016

Wakati joto la burudani likiendelea kupanda Kanda ya Ziwa kwa vipindi, habari na matangazo yenye mguso na jamii kupitia kituo cha redio Jembe Fm kinachorusha matangazo yake kutoka jijini Mwanza katika masafa ya FM 93.7, nayo safari ya kuelekea Tamasha kubwa la burudani linalojulikana kama JEMBEKA FESTIVAL 2016 linaufanya ukanda huo joto lake kupanda zaidi kiasi cha kusababisha presha kwa wadau wa Kanda husika. 

Jumamosi, May 21,2016 ndiyo siku litakapopigwa Tamasha la Jembeka Festival ikiwa ni Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja na Mkali Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Pia watakuwepo wasanii wengine kibao.


Wakati huo huo msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania ambaye historia ya muziki wa Bongo Fleva hainogi bila jina lake kutajwa, Juma Nature tayari ameangusha wino kuwa mmoja wa wasanii watakaomwaga burudani kwenye tamasha hilo.


Jina la Sir Nature lilihusishwa mapema kabisa katika mipango ya tamasha hilo kutokana na maombi ya mashabiki wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake kupitia ujumbe mfupi/sms za vipindi tofauti tofauti ndani ya Jembe Fm kiasi cha kuipa presha kamati husika kumuweka mkali huyo kwenye listi ya wakali watakaopanda jukwaa moja na Neyo.



 Licha ya msanii huyo kufanya makamuzi jijini Mwanza mapema mwezi Machi akipanda jukwaa moja na wakali wengine kutoka nchini Nigeria Tekno, Seyi Shey na Ommy Dimpoz kutoka nchini Tanzania nyota yake imeonekana kung'ara tena na tena kuelekea JEMBEKA NA VODACOM "Haijalishi mara ngapi ndani ya mwaka huu Nature kaja Mwanza na tukaenda kwenye show zake. Tunamtaka Nature!!" alisikika mmoja wa mashabiki wa burudani kutoka mkoani humo. 


List ya wasanii wengine watakao husishwa na tamasha hilo mpaka sasa bado haijatajwa rasmi,  licha ya fununu kwa baadhi ya wakali. 


Kumbuka ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 so anza kujichanga mapema mwana wa kwetu. Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Michuzi Blog, Binagi Blog na wadau wengine. 

Nunua Tiketi yako mapema www.jembenijembe.com

No comments: