JAJIMkuu
wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, amefanya ziara ya kikazi ya
kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika Kanda ya Mbeya.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande Othman akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Ziara
ya Mhe. Jaji Mkuu katika kanda hii imelenga kujionea hali ya utendaji
kazi wa Mahakama katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha
Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha
huduma ya utoaji haki nchini.
Katika
ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa
Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni
pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi
wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande Othman, (katikati) akipata taarifa fupi ya utendaji kazi wa
Mahakama Kanda ya Mbeya kutoka kwa Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi
Kanda ya Mbeya (aliyesimama), mara baada ya kuwasili katika kikao
kilichohusisha Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na
Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya.
Mhe.
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye alipata nafasi ya
kukagua na kuongea na Watumishi wa ngazi mbalimbali za Mahakama katika
mkoa huo.
Katika
kikao alichofanya na Watumishi wa Mahakama mkoani humo ikiwa ni pamoja
na Wahe. Majaji na Mahakimu, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza mara zote juu ya
utendaji kazi kwa kujituma ili kubadili taswira ya Mahakama kwa
wananchi ambao ndio wadau muhimu wa Mahakama.
Akiongea
na Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Jaji Mkuu alieleza
kufurahishwa na kasi ya usikilizaji na umalizwaji wa mashauri katika
Mahakama za Mwanzo mkoani humo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande Othman akizungumza na Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji,
Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya alipokutana nao na
kuwaasa kuendelea kutenda Haki kwa wakati ili kuweza kupunguza na
kumaliza mashauri yanayowasilishwa mahakamani.
Awali;
katika taarifa yake kwa Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. Noel Chocha, Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, alimtaarifu Mhe. Jaji Mkuu juu ya
mkakati waliojiwekea wa kumaliza mashauri ya aina yoyote kwa kipindi
kisichozidi miezi sita.
Aidha
Mhe. Jaji Mkuu alitumia ziara hiyo ya kikazi kuwaeleza Watumishi juu ya
mikakati ambayo Mahakama imejiwekea katika kuhakikisha kuwa huduma ya
utoaji haki inaboreshwa nchini.
“Kwa
hivi sasa Mahakama ya Tanzania imejiwekea mikakati/vipaumbele ambavyo
vinalenga kuboresha huduma ya utoaji haki nchini, na malengo haya
inabidi yafanyiwe kazi na kila mmoja wetu kwa maana ya kila Mtumishi na
mdau wa Mahakama awajibike katika kufikia malengo yetu ya kuboresha
huduma ya utoaji haki nchini.” Alisema, Mhe. Jaji Mkuu.
Uimarishaji
wa ukusanyaji wa takwimu; hili pia ni eneo ambalo limewekwa kama
kipaumbele katika maboresho Mahakamani, Mhe. Jaji Mkuu alisema Mahakama
pia imejipanga vyema kuhakikisha inakuwa na takwimu sahihi za kesi
mbalimbali zilizopo katika Mahakama mbalimbali nchini ili kuangalia ni
sehemu ipi inayohitaji nguvu zaidi katika kushughulikia mashauri/kesi za
muda mrefu.
Uboreshaji
wa Miundombinu: miundombinu hii ni pamoja na majengo ya Mahakama,
vitendea kazi n.k, Mhe. Jaji Mkuu alisema pia katika kuboresha huduma
zake Mahakama imejipanga katika kuboresha miundombinu yake ikiwa ni
pamoja na kujenga majengo ya Mahakama na kukarabati majengo
yaliyochakaa.
“Tatizo
kubwa ambalo Mahakama inakabiliana nalo ni uchakavu wa miundombinu
yake, kwa hili tuko mbioni kuhakikisha Mahakama inakuwa na miundombinu
bora zaidi, tumejipanga kuboresha ikiwa ni pamoja na kujenga Mahakama
Kuu katika mikoa yote ambao haina majengo, taratibu zinaendelea na kwa
mwaka huu tumepanga kuanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa ya Kigoma
na Musoma/Mara.
Uboreshaji
wa hali ya Wafanyakazi wa Mahakama; Hili pia ni moja kati ya eneo
ambalo limepewa kipaumbele katika maboresho yanayoendelea kufanyika
ndani ya Mahakama; Mhe. Jaji Mkuu aliwaeleza Watumishi wa Mahakama Mbeya
kuwa uboreshaji huu unaangalia upatikanaji wa stahili za Watumishi kwa
wakati ikiwa ni pamoja na nauli za likizo, madeni mbalimbali, uboreshaji
wa mishahara ya watumishi suala ambalo linaendelea kufanyiwa kazi.
Aidha
Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa suala Maadili na nidhamu pia limewekewa
kipaumbele, alisema kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Mahakama hawana
nidhamu na maadili katika utendaji kazi, hali hii imesababisha kuwa
Mahakama nzima kutupiwa lawana juu ya utendaji kazi wake.
“kuna
baadhi ya Watumishi ya watumishi wa Mahakama hawana maadili na nidhamu
hali hii inachafua taswira nzima ya Mahakama, lazima tuongeze uadilifu,
Watanzania wanataka Watumishi wanaotoa haki, wanaoaminika ili kila
mwananchi aridhike,” alisema.
Naibu
Msajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na
Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya waliokutana na kuzungumza na Jaji Mkuu
wa Tanzania kuhusu utendaji kazi Mahakama kwa Kanda ya Mbeya.
No comments:
Post a Comment